Saturday, January 30, 2016

Inauma sana--Mtu mmoja auwawa kwa kuchinjwa na kufungiwa ndani ya mashine ya kusaga nafaka Geita


Zoezi la usafi wa mazingira katika kijiji cha Muungano nje kidogo ya mji wa chato mkoani Geita limeingiwa dosali baada ya tukio la mtu mmoja kuuwawa kwa kuchinjwa na kufungiwa ndani ya mashine ya kusaga nafaka hali iliyosababisha mamia ya watu kufurika kushuhudia tukio la kusikitisha na kuacha kufanya usafi kwenye maeneo yao.


ITV imeshuhudia mamia ya watu wakiwa wamefurika katika mashine ya kusaga nafaka inayomilikiwa na Bi.Jamira Abdu Mkazi wa chato ambaye amemtaja marehemu kuwa anafahamika kwa jina la Juma Saidi alikuwa akifanya kazi ya kusaga nafaka katika mashine hiyo zaidi ya miaka saba na kusema kwamba hivi karibuni marehemu alikuwa na ugomvi na mkewake ambapo alihama nyumbani kwake na kuanza kulala mashineni hapo.
 
Baadhi ya wananchi wanaomfahamu marehemu Juma wamesikitishwa na tukio la mauaji ya kinyama na kuiomba serikali kuimalisha ulinzi na wengine wakuiomba kurejeshwa kwa jeshi la jadi Sungusungu kwa lengo la kukomesha matukio ya kihalifu.
 
Alipotakiwa kuthibitisha tukio hilo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Chato Bw. Shabani Ntalambe hakuwa tayali kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa anasimamia usafi wa mazingira ambapo ITV imelazimika kuzungumza na afisa mtendaji wa kijiji cha Muungano na diwani wa kata ya Muungano ambao wamethibitisha kutokea kwa mauaji ya kinyama

No comments: