Wednesday, January 6, 2016

Manispaa Ya Temeke Yazindua kijiko cha kuzolea Taka chenye Thamani ya Milllion 352

 Na Izack Magesa

HALMASHAURI ya Manispaa ya Temeke leo zindua rasmi kijiko cha kuzolea taka chenye thamani ya sh mil 352 ili kuboresha 

usafishaji wa mazingira wilayani humo kwa lengo la kuepuka magonjwa ya milipuko inayoweza kupelekea kupoteza maisha ya wananchi
wake.

Hata Hivyo Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalah Mtolea amewataka wananchi kushiriki katika utunzaji wa mazingira ili kuepuka mlipuko wa magonjwa kama kipindupindu.

"kikubwa wananchi  wapatiwe elimu  juu ya kuelewa umuhimu wa kutunza mazingira yao yanayowazunguka hivyo rai yangu  pia kwa wananchi kushiriki katika utunzaji wa mazingira ikiwa pamoja na kusafisha  maeneo yao"alisema.

Naye Afisa afya wa Manispaa ya Temeke Ali Khatibu alisema kuwa wastani wa taka zinazozolewa kwa siku ni tani 538 ambazo ni sawa na asilimia 47.3 ya taka zinazozalishwakwa siku wakati taka zinazosalia ni tani 599.5 ambazo ni sawa na asilimia 52 hivyo kuzinduliwa kwa kijiko hicho kitasaidia kuongeza uwezo wa uzoaji wa taka kufikia katika hatua nzuri ukilinganisha na hali ya sasa.
mwisho

 Akizungumza na Waandishi wa habari Dar es salaam jana,Mstahiki meya wa Halmashauri ya Temeke Abdalah Chaurembo alisema kuwa kufuatiauzunduzi wa kijiko hicho cha kuzolea taka kutachochea kwa kiasi kikubwa uboreshaji na kupunguza uchafu ndani ya wilaya yake ikiwa ni njia ya kutii na kutekeleza agizo la Rais Wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Alisema kuwa Halmashauri imejipanga vizuri katika kuhakikisha utekelezaji wa agizo lake la usafi wa mazingira linafakiwa kwa asilimia 100 hivyo ameziomba mamlaka husika wakiwemo maafisa afya wa kata na mitaa  kushirikiana kwa pamoja ili kudhibiti hali ya uchafu katika maeneo mbali mbali ya Temeke.

Wakati huo huo Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdalah Mtolea amesisitizia umuhimu wa wananchi kutambua utunzaji na usafishaji wa mazingira kwakuwa ni jambo linalotakiwa kupewa kipaumbele kwa kwa kiasi kikubwa ili kuepukana na magonjwa mbali mbali yanayohatarisha maisha ya jamii.




No comments: