Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mitihani ya kujipima ya darasa la nne huku matokeo hayo yakionyesha wanafunzi wengi wamefeli katika somo la Kiingereza kwa asilimia 65.67 katika mitihani hiyo iliyofanyika mwishoni 2015.
Akitangaza matokeo hayo leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde amesema juhudi za makusudi zinahitajika katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzia ili kuboresha kiwango cha ufaulu.
Jumla ya wanafunzi 869,057 kati ya wanafunzi 977,886 sawa na asilimia 88.87 waliofanya upimaji wamepata alama katika madaraja ya A,B,C,na D. Wanafunzi 108,829 sawa na asilimia11.13 wamepata alama za ufaulu usioridhisha.
Aidha wanafunzi wamefanya vizuri zaidi katika somo la Sayansi kwa asilimia 89.44, na baraza limewataka walimu kuweka mkazo zaidi kwa wanafunzi waliofanya vibaya ili wawasaidie kuimarika na waweze kupata ufaulu mzuri.
No comments:
Post a Comment