HATIMAYE Wahariri wa Gazeti la Mawio ambao walikuwa wanatufutwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Ya Dar es Salaam wamejisalimishwa kwenye Makao mkuu ya Kanda hiyo.
Wahariri hao ni Jabir Idrisa,Saimon Mkina wamejisalimisha mda wa saa 8.56 mchana jijini hapa,huku wakiongozana na Mwanasheria wa Gazeti hilo Frederick Kihwelo na Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri nchini (TEF),Absalom Kibanda,Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea,Aliyekuwa mhariri mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima,Ansbert Ngurumo.
Gazeti la Mawio ambalo lilifungiwa mwishoni mwa wiki iliyopita na Waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo ,Nape Nnauye kwa kutumia sheria ya magazeti ya mwaka 1976 kwa kusema kuwa Gazeti hilo lilikuwa linaandika habari za uchochezi.
Akizungumza nje ya Polisi hapo mara baada ya wahariri hao kujisalimisha,Mwenyekiti wa TEF,Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Mtanzania,Dimba,Rai nguvu ya hoja,The African,Bingwa,amewambia waandishi wa habari, kuwa wao kama (TEF) wamekuja kumsindikiza mhariri mwenzao polisi hapo kwa madai kuwa ni miongoni mwa wajumbe kwenye jukwaa hilo.
“Tumekuja kuwasindikiza wenzetu hawa kwakuwa ni wajumbe wa TEF,tumekuja pia kujua sababu gani ya polisi kuwaita wahariri hawa”amesema Kibanda.
Hata hivyo Kibanda alitumia nafasi hiyo kutoa masikitiko yake kwa hatua iliyochukuliwa na serikali kwa kulifuta Gazeti la Mawio kwa kusema serikali inanyima uhuru wa habari kwani wao kama TEF hawaoni kosa walilofanya Gazeti hilo mpaka kupewa adhabu hiyo kubwa.
“Tumesikitika sana na hatua hii ya kikandamizaji ya kulifungia Gazeti la Mawio na huu ni mwendelezo wa serikali kunyima uhuru wa habari nchini,na sisi jukwaa la wahariri hatutakubali kufanya kazi na waziri wa aina hii na tutatoa tamko ngojeeni”amesema kibanda.
Kwa upande wake Mbunge wa Ubungo wa Saed Kubenea,ambaye pia ni mkurugenzi wa Kampuni ya Hali halisi limited ambayo inamiliki Gazeti la Mwanahalisi,Mtandao wa Mwanahalisi oline,Gazeti la Mseto,amesema amekuja Polisi hapo ili kwasababu miongoni mwa wahariri alishikiliwa na polisi ni mfanyakazi wake.
“Huyu Jabir ambaye amejisalimisha leo ni mfanyakazi wangu kwenye Gazeti la Mwanahalisi na nimeshangaa kwanini leo polisi naye wamemkatamata hili ni jambo la ajabu sana na huu ni uonevu unaofanywa na serikali ili kutaka kuwaziba wanahabari mdomo wasisema mambo mabaya kwa serikali”amesema Kubenea.
Kubenea amezungumzia hatua ya serikali kulifungia gazeti la Mawio kwa kusema Waziri Nape amekurupuka na anafanya kazi ya katibu uenezi wa chama cha Mapinduzi CCM kwenye nafasi ya uwaziri.
“Huyu Waziri amekurupuka tu hakuna kosa lolote Gazeti lilofanya,anasema Gazeti limeandika uchochezi, hivi wanahabari mtu wakusema habari hii ni ya uchochezi ni Mahakama na sio waziri wa habari,nashangaa yeye anasema tumeandika uchochezi wakati sio mahakama”amesema Kubenea.
Kubenea ameongeza kuwa Waziri Nape anapodai Gazeti la Mawio linaandika Uchochezi amedai kuwa ni uongo wa mchana kwani kama lingekuwa linaandika uchochezi mbona waziri huyo alikuwa anaandika habari kwenye gazeti hilo.
“Huyu Nape leo anafanya kugeuka mbona alikuwa mwandishi wa habari wa Gazeti la Mwanahalisi kama lingekuwa linaandika uchochezi mbona alikuwa anaandika habari kwetu,harafu nataka niwaambieni huyu Nape ni source (Chanzo) mzuri kwenye Gazeti letu hebu muulizeni.
Mpaka Mwandishi wetu anaondoka makao makuu ya polisi kanda maalum ya Dar es salaam Wahariri hao walikuwa bado wapo kwenye Mahojiano
No comments:
Post a Comment