Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi akipongezana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye wakati wa mkesha maalum wa kuombea taifa uliofanyika uwanja wa Taifa usiku wa kuamkia leo.
………………………………………………………………………………………………………..
Na Magreth Kinabo – MAELEZO
Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuwaombea watu wenye nia mbaya na Taifa la Tanzania ili waweze kuwa raia wema na kuachana na tabia za kutaka rushwa, uvivu, uzembe na matumizi ya dawa za kulevyia.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mgeni rasmi kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika maombi maalum ya kuliombea dua Taifa na viongozi, ambaye ni Waziri Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dares Salaam.
“Tabia hizi zimeota mizizi zinahitaji maombi. Tunao uwezo wa kumwuunga mkono Rais. Kila mtu anao mchango wa kumsaidia Rais anayoyafanya mfano katika vijiji kutumbua majibu madogo,” alisema Lukuvi .
Aliongeza kwamba viongozi hao wanapaswa kuelimisha jamii jinsi ya kufanya kazi kwa bidii, hivyo wasiache kusisitiza juu ya suala hilo, likiwemo suala la, amani upendo umoja na mshikamano.
“ Misingi hii ya, upendo, umoja na mshikamano ilianzishwa na Serikali zilizopita na Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuhimiza juu ya misingi hii, bila ya kujali dini , rangi, kabila, itikadi na eneo analotoka mtu,” alisisitiza.
Alisema uhuru wa kuabudu utaendelea kuwepo, ila kwa kuzingatia sheria zilizopo.
Aidha Waziri Lukuvi alisema Serikali itaendelea kutoa fursa sawa za kiuchumi na kijamii kwa wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya wa Makanisa ya Pentekoste, ambaye pia ni Askofu wa Huduma ya Tanzania Fellowship Churches (TFC), Askofu Godfrey Malassy alisema wao kama viongozi wa dini wako pamoja na Rais John Pombe Magufuli, hivyo hawatamwacha pekee yake katika mapambano hayo hadi Tanzania itakapokuwa mahali penye neema pa kuishi.
Askofu Malassy aliongeza kwamba ni wajibu wa Watanzania kuomba ili kuweza kuleta mabadiliko katika Taifa letu.
Alisema madhuni ya maombi hayo ni kumwombea Rais Magufuli aweze kuendelea kuliongoza Taifa ili liweze kuwa na maendeleo ya ustawi wa watu wote na liendane na kasi ya kauli mbiu ya ‘Hapa Kazi tu!.
Askofu huyo alisema mauzo ya kitabu cha ijue siri ya amani na sadaka zitakazotokana na mkesha huo zitatumika kuelimisha jamii ya ya umuhimu wa amani, kuendelea kutoa huduma hiyo kwene mikoa ambayo hawajaifikia na kugusa jamii yenye mahitaji maalum hasa wakina mama na watoto kwa kusaidia kutoa huduma ya nishati ya umeme
No comments:
Post a Comment