Vyombo vya ulinzi
nchini pamoja na seriali kwa ujumla wametakiwa kuelewa kuwa vitendo vya ugaidi
vinavyotokea nchini Poamoja na duniani kwa ujumla havina uhusiano wowote na
dini ya kiislam kama jinsi ilivyokaririwa na wengi hivyo dini zote nchini ziaminiane
na kupiga vita vitendo vyote vya kigaidi duniani.
Kiongozi mkuu wa madhehebu ya shia nchini Sheikh HEMED JALALA akizungumza na wanahabari leo |
Hayo yemeelezwa leo
katika semina iliyowakutanisha waumini wa dini ya kiislam kwa pamoja
iliyoandaliwa na taasisi ya Imam Buhar Islamic Foundation iliyokuwa na lengo la
kujadili kwa pamoja changamoto zinazoikumba dini ya kiislam kwa sasa hususani
swala la ugadi ambalo limeendelea kuwa tishio kwa kizazi cha sasa.
Akizungumza na mtandao
huu mwenyekiti wa Imam Buhari Foundation ambao ndio waandaaji wa semina hiyo
iliyofanyika jijini Dar es salaam SHEIK KHALIFA KHAMIS amesema kuwa dini ya
kiislam haina mahala popote inapofundisha watu wake mafunzo ya
kigaidi,mauaji,na vitendo vya kinyama vinavyotendeka duniani hivyo ni lazima
watanzania na dunia kwa ujumla kuacha kuamini kuwa vitendo vya kigaidi
vinafanywa na waislam.
“Leo akipatikana mtu
mmoja ambaye kavaa kanzu kafanya vitendo vya kigaidi basi inachukuliwa kuwa
waislam woote ni magaidi dunian,sio kweli na hatufundishi ugaidi katika dini
zetu,tunaomba vyombo vya dola kufuta mawazo haya mabaya juu ya uislam”amesema.
Waislam waliohudhuria semina hiyo wakisikiliza kwa makini |
Ameongeza kuwa semina
hiyo imekuja mahususi kuwakumbusha waislam jukumu lao la kujenga umoja miongozi
mwao na kwa watanzania kwa ujumla jambo ambalo litasaidia katika kuendeleza
umoja na mshikamano wa watanzania uliopo.
Aidha katika hatua
nyingine naye Kiongozi mkuu wa madhehebu ya shia nchini Sheikh HEMED JALALA
akizungumza na wanahabari ameipongeza taasisi ya Imam Buhar kwa kuandaa semina
hiyo ambayo amesema imekuja wakati muafaka ambao vitendo vya ugaidi vimeshika kasi
sana katika nchi nyingi jambo ambalo linaendelea kuzua hofu kwa dunia nzima.
Baadhi ya picha zinazoonyesha madhara ya vitendo vya kigaidi duniani |
Amesema kuwa nchi ya Tanzania
ni moja kati ya nchi chache duniani ambazo zinaishi kwa umoja na mshikamano
pamoja na upendo wa hali ya juu hivyo semina hiyo itatumika kuwatahadharisha
watanzania kuepuka sana kukaribisha vitendo vya kigaidi katika nchi yao kwani itasababisha
hatari kubwa.PICHA ZOTE ZA SEMINA HIYO ZIPO CHINI BOFYA
No comments:
Post a Comment