Tuesday, February 2, 2016

Mvua yaleta maafa Tandahimba,kaya 63 zakosa makazi na chakula

Mbunge w jimbo l Tandahimba KATNI KTNI liyev shati la njano akiwa na Diwani wa kta y kwanyama MOHMED OSI wakingalia moja ya nyumba zilizoezuliwa na mvu hiyo ambapo kaya 63 zimekosa makazi na chakula

 Haika Kimaro.
Tandahimba.Zaidi ya kaya 63 kata ya Kwanyama wilayani hapa zimekosa chakula na makazi baada ya nyumba zao kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua hapo juzi.
Hali hiyo imetokea ikiwa ni wiki 3 zimepita tangu tukio na aina hiyo kutokea kata ya Chaume wilayani hapa na kuaziacha kaya nyingine zaidi ya 100 kukosa makazi na chakula pamoja na mikorosho 400 kuharibiwa.
Akizungumza diwani wa kata ya Kwanyama,Mohamed Osi amesema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa9 alasiri baada ya mvua kali kunyesha ikiambatana na upepo ulioenzua mapaa ya nyumba na kusababisha baadhi ya nyumba kubomoka kwa kiasi.

"Tukio hili lilitokea juzi majira ya saa9 zaidi ya nyumba 64 ziliezuliwa na vyakula vilivyokuwemo ndani kuharibika sambamba na miti ya mikorosho na ndizi kuharibika,hivyo tunawaomba wahisani watusaidie,"alisema Osi
Hata hivyo baada ya tukio hilo mbunge wa jimbo la Tandahimba,Katani Katani aliweza kuwatembelea waathirika wa maafa hayo na kutoa msaada wa bati 300 zenye thamani ya 3.6 milioni ili kuwawezesha wananchi hao kurudisha makazi yao.
Akizungumza alisema kuwa "Tangu niingie madarakani hili ni tukio la pili linatokea kwenye jimbo langu,juzi nilipigiwa simu na diwani kunipa hizi taarifa wakati nikiwa bungeni na leo nimekuja kuwaona na kuwapa pole na nitakabidhi hapa bati 300,"alisema Katani na kuongeza

"Wakati wa siasa umepita sasa kikubwa ni kuangalia suala la maendeleo ya Tandahimba,"alisema Katani
Akizungumza mkuu wa wilaya ya Tandahimba,Emmanuel Luhahula,alisema kamati ya maafa tayari inaendelea kufanya tathmini sambamba na kugawa chakula cha msaada kwa.waathirika.
Hata hivyo alisema hadi kufikia jana katika wilaya yake watu wapatao watano wamefariki kutokana na matukio ya radi.
Mbunge wa jimbo la Tandahimba Mh KATANI KATANI akiwakabidhi baadhi ya msada wa mabati 300  waathirika wa maafa hayo,bati zenye thamani ya milion 3.6
Alisema waliofariki ni mwananfunzi wa shule ya msingi Kunandundu baada ya radi kupiga wakati wakiwa shuleni na wengine kujeruhiwa na kulazwa hospitali ya wilaya,watoto wawili wa familia moja,na wanawake wengine wawili.
"Taarifa ya maafa ninayo na kamati yangu ya maafa ipo inaendelea na kazi kufanya tathmini kuona wale watu wanasaidiwaje lakini pia wanaendelea kupewa msaada wa chakula,"alisema Luhahula
Wakizungumza waathirika wa maafa hayo,Radhia Saidi na Hassan Ally wameziomba taasisi nyinginezo na wanajamii kujitolea kuwapatia msaada ili kunusuru maisha yao na kudai kwa sasa wanalazimika kulala kwa watu kutokana na makazi yao kuharibika.
Mratibu wa maafa wilaya,Rajab Yasin alisema waliobomolewa nyumba wamehifadhiwa kwa ndugu zao na tathmini bado inaendelea na pale itakapokamilika itawasilishwa halmashauri na kueleza kuwa kamati hiyo pia inaendelea na ugawaji wa chakula ambapo kaya moja inapatiwa unga kg 25,maharage kilo 5 na chumvi pakti moja.



No comments: