Kesho Jumamosi, Yanga SC watakua wenyeji wa APR ya kutoka nchini Rwanda katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa (CAF CL) kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, mchezo utakaochezeshwa na mwamuzi Bernard Camille, akisaidiwa na Eldrick Adelai, Gerard Pool na Allister Bara kutoka nchini Shelisheli.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri vilabu wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, timu za Azam FC, JKU na Yanga SC katika michezo yao watakayocheza wikiendi hii.
Katika salamu hizo, TFF imezitakia kila la kheri timu hizo kuhakikisha zinafanya vizuri katika michezo yao ili ziweze kusonga mbele katika hatua inayofuata, na kuwapa furaha washabiki wa mpira wa miguu pamoja na watanzania wote.
Timu ya JKU ya visiwani Zanzibara leo Ijumaa watakua kibaruani kuchuana na SC Villa ya Uganda, mchezo utakaochezwa katika uwanja wa Amani mjini Zanzibar.
Jumapili Azam FC watakua wakicheza dhidi ya Bidvest FC kutoka nchini Afrika Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (CAF CC) kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, mwamuzi wa mchezo huo ni Gait Oting akisaidiwa na Abdallah Gassim, Casim Dehiya, mwamuzi wa akiba Ariel James wote kutoka Sudan Kusini
No comments:
Post a Comment