Tuesday, March 15, 2016

LIGI KUU KUENDELEA JUMATANO


Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumatano kwa mchezo mmoja, ambapo Azam FC watawakaribisha Stand United katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Ijumaa mkoani Shinyanga katika uwanja wa Kambarage, wakata miwa wa Kagera Sugar watakua wenyeji wa ndugu zao kutoka wakata miwa Mtibwa Sugar kutoka Manungu Turiani.
Wikiendi Jumamosi na Jumapili ligi hiyo itaendelea kwa michezo mitano kuchezwa katikwa viwanja mbalimbali nchini, jijini Tanga wenyeji Coastal Union wakiwa wenyeji wa Simba SC katika uwanja wa Mkwakwani jijini humo.
Majimaji FC itakua nyumbani katika uwanja wa Majimaji mjini Songea kucheza na Mbeya City, huku chama la wana Stand United wakiwakaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Jumapili African Sports watakua wenyeji wa maafande wa jeshi la magereza Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Mkwakwani jijii Tanga, huku siku ya Jumatatu Mgambo Shooting wakicheza dhidi ya Toto Africans jijini Tanga katika uwanja wa Mkwakwani.

No comments: