Friday, March 4, 2016

TIGO YATOA UDHAMIN WA MILIONI 11 KAMPENI YA ‘KUTOA AHADI YA UWIANO WA KIJINSIA”

 Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha (Kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya udhamini wa Tigo wa kiasi cha Shilingi Milioni 11 katika kampeni ya  ‘KUTOA AHADI YA UWIANO WA KIJINSIA  ambayo inatarajiwa kuanza na matembezi ya kilomita 6 ambayo yataanzia kwenye  “Uwanja wa Mbio za Mbuzi”, Masaki, Dar es Salaam Jumamosi Machi 5 saa 12 asubuhi, katikati Mwenyekiti wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA), Sadaka Gandi na kushoto  ni Rais wa  (TWA,) Irene Kiwia   ambao ndio waandaaji wa matembezi hayo, kwenye mkutano uliofanyika mapema jana  jijini Dar es salaam.
Rais wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) Irene Kiwia  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu udhamini wa Tigo katika  kampeni ya kampeni ya  ‘KUTOA AHADI YA UWIANO WA KIJINSIA ni kauli mbiu kuelekea kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, inatarajiwa kuanza na matembezi ya kilomita 6 ambayo yataanzia kwenye  “Uwanja wa Farasi ”, Masaki, Dar es Salaam Jumamosi Machi 5 kwenye mkutano uliofanyika mapema jana  jijini Dar es salaam. 

Mwenyekiti wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA),) Sadaka Gandi (katikati)  akifafanua jambo kuhusu  uzinduzi wa kampeni ya kampeni ya  ‘KUTOA AHADI YA UWIANO WA KIJINSIA  kushoto kwake ni  Meneja Mawasiliano wa Tigo John Wanyancha na kushoto kwake Rais wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) Irene Kiwia kwenye mkutano na waaandishi wa habari uliofanyika mapema jana jijini Dar. (P.T)

Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Rais wa  TWA Irene Kiwia kuhusu udhamini wa Tigo katika  kampeni yakampeni ya  ‘KUTOA AHADI YA UWIANO WA KIJINSIA  ambayo ni kauli mbiu kuelekea kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani katika mkutano uliofanyika mapema jana Jijini Dar es salaam .

 Kampuni  ya Tigo Tanzania  imedhamini kampeni ya Kutaka Uwiano ambayo inatarajiwa  kuanza na matembezi ya kilomita sita ambayo yataanzia kwenye “Uwanja wa Mbio za Mbuzi”, Masaki, Dar es Salaam Jumamosi Machi  5, 2016.
Kampeni hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Wanawake wenye Mafanikio (TWA) ambayo ni asasi isiyo ya kiserikali
ambayo lengo lake kuu ni kuimarisha ushiriki, na majukumu yawanawake na uwezo wao katika jamii ya Tanzania kwenye mambo ya kijamii, kisiasa na kiutamaduni.


Kutoa    Ahadi ya Uwiano wa kijinsia ni kauli mbiu ya mwaka huu katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake. Ambayo kilele chake kitakuwa Machi 8, 2016.Kampeni ya Kutoa Ahadi ya Uwiano wa jinsia inatoa wito kwa kila mtu kuchukua hatua za dhati kusaidia upatikanaji wa uwiano wa kijinsia kwa kasi zaidi ilikuwa saidia wanawake na wasichana kufikia  matamanio yao.

Matembezi hayo ya tafuatiwa na Kongamano la Siku ya Kimataifa ya Wanawake litakaofanyika kwenye Hoteli ya
Regency Kilimanjaro, Jumapili, Machi 6. Akizungumza  kwenye mkutano  wa waandishi  wa habari jana jijini Dar es salaam, Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha alisema kwamba kama kampuni ya maisha ya kidijitali Tigo inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wanawake ndani ya jamii na ndio maana  kampuni hiyo inaungana na watu wenye mapenzi mema kuunga mkono kampeni  ya TWA.


 “Tigo inajivunia kuunga mkono TWA kwenye kampeni hii ambayo ambayo inatafuta kuwawezesha wanawake kuingia kwenyeustawi wa wasaidie wengine kustawi kwa ajili ya manufaa ya jamii. Ikiwa ni kampuni inayoendeshwa kwa ubunifu, Tigo iko tayari kufanya kazi na watu wengine ambao ni  wabunifu, jamii, asasi zisizo za serikali, serikali, sekta binafsi na za umma kwa ajili ya manufaa ya jamii yote,” alisema Wanyancha.

Akitoa shukrani zake kutokana na kuungwa mkono huko,Rais wa  TWA, Irene Kiwia aliishukuru Tigo kutokana na kujikita kwake kusaidia mikakati mbalimbali ambayo imejielekeza katika kuisaidia  jamii.

Kiwiaalisema, “Wakati tunakaribia kuanza Kampeni ya Kutoa Ahadi ya Uwiano wa kijinsia,tunapenda kuishukuru Tigo kwa ukarimu wake wa kutuunga mkono.

Bila uungwaji mkono wa kampuni hii pamoja na huduma zake kubwa hatungeweza kufikia malengo yetu mengi katikakupanga na kuandaa kampeni hii. Uungwaji mkono wa Tigo utakuwa na matokeo ya muda mrefu yatakayowanufaisha wanawake kufuatia mafanikio ya kampeni hii.”

Hali kadhalika Kiwia alitoa wito kwa watu kushiriki kwenye Matembezi ya Kutoa Ahadi ya Uwiano wa kjiinsia akisema, “Tunatoa wito kwa watu binafsi, asasi zisizo za serikali, vyombo vya  habari, maofisa wa sekta  za umma na binafsi na wadau wengine kuja kwa wingi na kuungana na sikushiriki kwenye matembezi na waalikwa kushiriki kwenye Mkutano wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake.

NaibuWaziriWaAfya, Maendejana ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Hamisi Kigwangala, atakuwa mgeni
rasmi katika matembezi   hayo.  Licha ya kutoa suluhisho la kiteknolojia kidijitali la kisasa hapa nchini, Tigo kwa miaka mingi imekuwa ikisaidia mikakati  ya kijamii ambayo yanaleta manufaa makubwa kwa  jamii.

No comments: