Naibu waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya akishiriki matembezi ya maadhimisho ya siku ya watu wenye usonji Duniani ambayo imeadhimishwa leo Jijini Dar es salaam |
Na Exaud Mtei (Msaka Habari)
Serikali ya Tanzania imesisitiza
kuwa itaendelea kutoa elimu bora na Bure kwa watoto wote wa kitanzania bila
kubagua rangi,kabila wala dini huku mkazo mkubwa sasa ukielekezwa pia kwa
watoto wenye ulemavu na mahitaji maalum lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa watoto
wote wa Tanzania wanapata elimu sawa.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Dar es salaam na Naibu
waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Manyanya wakati akisoma hotuba
ya Makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mama SAMIA SULUHU wakati
akimwakilisha katika maadhimisho ya siku ya watu wenye usonji duniani ambayo
huazimishwa kila mwaka tarehe mbili ya mwezi wanne.
Akisoma hotuba hiyo Eng
Manyanya amesema kuwa serikalI ya awamu ya tano chini ya Rais DR JOHM MAGUFULI
imedhamiria na imeamua kutoa elimu bure katika ngazi ya elimu ya msingi pamoja
na kupanua fursa ya elimu kwa watoto wenye uhitai maalum kwa kuandaa walimu,kuboresha
miundo mbinu na kutoa kipaumbele kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika
elimu.
Mhe. Dr. POSSY Abdallah. Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu Mkuu Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu...akishiriki matembezi hayo leo Jijini Dar es salaam |
Aidha katia maadhimisho
hayo ambayo yameandaliwa na taasisi ya Khoja Shia Itha Asheri Jamaat na
kufanyika katika viwanja vya shule ya AL MUNTAZARI Mh Naibu waziri ameipongeza
sana taasisi hiyo kwa kufanikiwa kuwa msatari wa mbele katika kuwahudumia
watoto wenye matatizo ya Usonji na mahitaji mengine maalum kwa kuwapatia Elimu
kulingana na mahitaji yao,ambapo amewataka wadau mbalimbali wakiwemo Walezo,wazazi
na taasisi nyingine kuunga mkono juhudi hizo ili kuwajenga watoto hao waweze
kuwa msaada katika taifa la Tanzania.
Usonji ni upungufu wa
kibaiologia anaopata mtoto anapokuwa tumboni kwa mama yake na dalili zake
huonekana kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea ambapo.
Maadhimisho ya watu
wenye usonji huazimishwa kila tarehe 2, ya mwezi april ambapo kauli mbiu ya
mwaka huu ilikuwa “TUWAPENDE NA TUWALINDE.Picha zaidi Bofya chini
Mhe. Dr. POSSY Abdallah. Naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu Mkuu Sera, kazi, Ajira, Bunge, Vijana na walemavu... |
No comments:
Post a Comment