Afisa elimu taaluma secondari, Justine Machela akiwa katika maktaba ya kompyuta katika shule ya Shangani manispaa ya Mtwara baada ya kukabidhiwa na shirika la Koica kwa udhamini wa serikali ya Korea ya kusini,Kushoto ni meneja wa Koica Tanzania,Lee Eun Ju na kushoto ni mkuu wa shule hiyo, Sophia Haule.
Shirika hilo limekabidhi maktaba ya vitabu na kompyuta jumla kuu ni Sh55,171,080
Na mwandishi wetu Mtwara
Tatizo la uhaba wa vitabu lililokuwa likiwakabili wanafunzi wa shule ya sekondari ya Shangani manispaa ya Mtwara Mikindani limekwisha baada yaserikali ya Korea ya kusini kupitia shirika la Koica kukabidhi maktaba ya vitabu na komyuta vyenye thamani ya Sh 55,171,080.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa maktaba hizo mkuu wa shule ,Sophia Haule alisema kupatikana kwa maktaba hizo kumeondoa tatizo la uhaba wa vitabu lililokuwepo awali na sasa wanafunzi watapata fursa ya kuzitumia na kutumia kompyuta kujitafutia notisi tofauti kwaajili ya masomo yao.
“Siku za nyuma vitabu vilikuwa vichache sana lakini sasa tumepata vitabu 2,500 ambavyo ni vingi,kwasababu awali vilikuwa vichache na tulikuwa tunavifungia kabatini kutokana na kukosekana kwa maktaba na wanafunzi kukosa fursa ya kuvitumia wakiwa katika mazingira ya shule na komputa baada ya kuweka huduma ya mtandao itawasaidia kutafuta material,”alisema Mwal Haule
Akizungumza meneja wa Koica nchini, Lee Eun Ju alisema kuwa kuanzishwa kwamaktaba hizo ni jitihada za kuiunga serikali mkono katika kuboresha elimu na kuwasaidia watoto kutimiza ndoto zao baada ya kuona shule hiyo ilikuwa na changamoto ya ukosefu wa maktaba na kompyuta.
“Awali tulikuja kwaajili ya kufundisha lakini tukaona kuna changamoto ya maktaba na kompyuta na maktaba ya mkoa gharama zake zilikuwa kubwa hivyo tukaandika mradi kuomba msaada ili kutengeneza maktaba za vitabu na kompyuta ambazo wanafunzi watazitumia kujisomea,”alisema Lee Eun Ju
Kwa upande wake afisa elimu taaluma sekondari, Justine Machela kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa alisema kuwa vitabu hivyo pamoja na kompyuta vitasaidia kuziba pengo la vitabu na uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi kwa kuongozwa na walimu wachache waliopo na kushukuru serikali ya Korea kusini kupitia shirika shirika la Koica.
“Umuhimu wa maktaba ni mkubwa kwasababu maktaba ni kama mwalimu aliyesimama pale wakati wote,ambapo mwanafunzi anapokutana na kikwazo anarudi maktaba na kutafuta kile anachokihitaji, na ukiangalia walimu wa sayansi ni wachache hivyo ni jukumu la walimu wale wachache waliopo kuwahimiza wanafunzi kuingia maktaba kusoma,”alisema Machela
Aidha aliwataka wanafunzi hao kutumia kompyuta hizo vizuri na kuzitunza ili kusaidia na vizazi vijavyo katika masomo yao.
“Awali Koica walituletea walimu tukajua watafundisha pekee lakini wameweza kuona jitihada zinazofanywa na serikali juu ya elimu na wao wakaamua kutuunga mkono,kikubwa niwasisitize walimu kuwahimiza wanafunzi kuingia maktaba kusoma na kutumia kompyuta kwaajili ya masomo na wazitunze vizuri,”alisema
|
No comments:
Post a Comment