Mkuu wa Wilaya ya Mpwawa iliyopo mkoani Dodoma, Mohamed Utaly (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu harambee ya kupata fedha za kununulia madawati itakayofanyika Juni 4 mwaka huu Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Donald Ngwenzi,Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Maje na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, Samuel Albertus Coy.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Mohamed Maje (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Donald Ngwenzi, akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mohamed Utaly.Na Dotto Mwaibale
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mpwapwa Dodoma Juni 4 mwaka huu inatarajia kufanya harambe ya kupata fedha za kununulia madawati kwa ajili ya shule za msingi na sekondari wilayani humo ambayo itafanyika Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi Mkuu wa Wilaya hiyo Mohamed Utaly alisema wamefikia hatua hiyo ili kukabiliana na uhaba wa madawati katika shule hizo ambapo pamekuwa na changamoto kubwa.
Alisema awali halmashauri hiyo ilikuwa na upungufu wa madawati 16,000 lakini baada ya kuwashirikisha wananchi na kufanya harambee mbalimbali walifanikiwa kupata madawati 6000 na kubaki kiasi cha madawati 10,000 ambayo yanahitaji.
Utaly alisema halmshauri hiyo katika bajeti yake ya mwaka 2015-2016 ilitenga sh. milioni 180 kwa ajili ya madawati ambapo kunamafanikio makubwa ya kupata madawati hayo yaliyosalia hivyo akatumia fursa hiyo kuwaomba wadau mbalimbali wa ndani wa wilaya hiyo na nje kujitokeza katika harambee hiyo ili waweze kufanikisha jambo hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mohamed Maje alisema changamoto kubwa waliyoibaini ni kutokuwa na kitengo cha kufanya ukarabati wa madawati yaliyo haribika ambacho hivi sasa kimeanzishwa.
"Kwa muda mrefu hatukuwa na kitengo cha kukarabati madawati yaliyoharibika lakini sasa tumekianzisha na kitasaidia kupunguza changamoto hiyo kwa kitengo hicho kitakuwa kikisaidia na wajasiriamali waliopo kwenye vikundi vya watu 20 ambavyo vipo sita kwa ajili ya kufanya kazi hiyo" alisema Maje.
No comments:
Post a Comment