Baada ya ukimya wa muda
mrefu nchini Tanzania kuhusu upatikanaji wa katiba mpya ambayo mchakato wake
ulitelekezwa na serikali ya awamu ya nne hatimaye Jukwaa la katiba nchini
Tanzania JUKATA wameamua kufufua upya mchakato huo huku wakimtaka Rais wa Sasa DR
JOHN POMBE MAGUFULI kutangaza haraka kuanza kwa mchakato wa katiba mpya na
kuacha kuona ugumu katika swala hilo nyeti kwa wananchi.
Mchakato wa katiba mpya
nchini Tanzania uliasisiwa na Aliyekuwa Rais wa Awamu ya nne Mh Dr JAKAYA
KIKWETE ambapo pamoja na changamoto nyingi kujitokeza mchakato huo ulizalisha
Katiba inayopendekezwa ambapo hadi leo haijulikani ni lini mchakato huo
utaendelea ili kuwapatia watanzania katiba mpya.
Akizungumza na
wanahabari Leo Jijini Dar es salaam mwenyekiti wa Jukwaa la katiba Tanzania
Jukata Bwana DEUS KIBAMBA amesema kuwa
Serikali ya awamu ya Tano imekuwa waoga kuhusu mchakato huo huku Rais
akishindwa wapi pa kuanzia kutokana na jinsi mchakato huo ulivyoendeshwa hapo
awali jambo ambalo limewasukuma wao kama JUKATA kauamua kuingia Rasmi katika
kufufua mchakato huo ambao umetafuna mabillioni mengi ya watanzania.
Bwana KIBAMBA ameeleza
kuwa wananchi wengi wamekuwa wakifwatilia kwa ukaribu swala la katiba mpya na
kuishia kuwahoji wao kuwa umeishia wapi hivyo wameamua kuwasaidia wananchi
kufufua mchakato wao ambao umetafuna pesa zao ili kuwasaidia kupata katiba
mpya.
“Tunatangaza Rasmi kuwa
leo kwa upande wa wananchi tumezindua Rasmi mchakato wa kudai katiba mpya
nchini Tanzania na tunaitaka serikali kupitia kwa waziri wa Sheria na Rais kwa
ujumla warejeshe mchakato wa katiba mpya ili watanzania wapate katiba ambayo
iliwapotezea muda katika kutoa maoni.
Ameendelea kueleza kuwa
Rais wa awamu ya Tano amesikika akitaja neno katiba mpya mara mbili tu tangu
alipoingia madarakani jambo ambalo amedai ni hatari sana kwa mchakatro huo
kutokana na uhitaji wa katiba kwa wananchi na gharama zilizotumika.
Aidha Jukwaa la katiba
Tanzania limeitaka serikali kupitia kwa wizara ya katiba na sheria kupeleka
bungeni mishwada ya kurekebisha sheria zinazosimamia mchakato wa katiba kwa
ajili ya kuhuisha katika tarehe zake zote zilizopitwa na wakati hii ni kutokana
na sheria ya mabailiko ya katiba ya mwaka 2011 na ile ya kura ya maoni ya 2013 kupitwa
na wakati na haziwezi kutumika tena bila marekebisho na kwa vile bunge la
bajeti linaelekea kumalizika bila mishwada ya marekebisho ya sheria hizo kupelekwa
bungeni na hakuna pesa iliyotengwa kwa ajili ya swala la katiba mpya katika
bajeti ya mwaka huu.
Aidha Jukata
wamependekeza kuitishwa kwa mkutano mkuu wa kitaifa wa katiba maarufu kama
NATIONAL CONSTITUTION CONFERENCE ambao utatumika kupitia maudhui ya katiba
iliyopendekezwa ilinganishwa na Rasimu ya tume ya warioba lengo likiwa ni
kuainisha maeneo makuu yanayolalamimikiwa na watanzania kiasi cha kuligawa Taifa
kama nilivyo sasa.
Jukwaa la katiba
Tanzania JUKATA wamekuwa kimya tangu kuingia kwa serikali ya awamu ya tano
ambapo sasa wameibuka na kudai kuwa wamegundua serikali hii imekuwa waoga wa
kuendeleza mchakato wa katiba na wao wameamua kuamsha watanzania na sasa
wataingia mtaani kutoa elimu na kuamsha hari ya watanzania kudai katiba yao
ambayo imetumia mabilion katika ukusanyaji wa maoni yake.
No comments:
Post a Comment