Leo
ni siku ya tarehe 23 mwezi june ambako duniani kote uadhimishwa siku ya wajane
duniani na kwa mara ya pili Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku hiyo. Leo wajane
zaidi ya 500 walikuwa katika uwanja wa mnazi mmoja kwa kuadhimisha siku yao
chini ya chama chao cha wajane (TAWIA) wajane hao wameweza kuadhimisha siku
hiyo kwa tafrija fupi iliyo udhuriwa na vyama mbalimbali vinavyotetea haki za
wanawake na nyinginezo kama WLAC,ISF,LHRC,UN na vyama vingine vingi vinayosaidia kupatikana
kwa haki za wajane.
SIHABA MKINGA – KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII YA JINSIA WAZEE NA WATOTO. akizngumza katika maadhimisho hayo |
Siku
hiyo iliyopambwa na mambo mbalimbali yaliyofanyika uwanjani hapo kama maigizo
yaliyofanywa na wajane wenyewe wakiweza kuonyesha jinsi gani wanavyoweza kupata
manyanyaso baada ya wanaume wao kuweza kufariki dunia na ndugu wa mwanaume
kusahau kuwa ndugu yao ameacha mjane na watoto na hivyo kuchukua mali zote bila
kufikiria mjane na watoto walioachwa wataishi vipi pia kuliweza kuwa na nyimbo
mbalimbali walizoziimba kwa majonzi wakielezea upatikanaji wa haki zao.
Sherehe
hiyo iliyoudhuliwa na wageni toka sehemu mbalimbali akiwemo SIHABA MKINGA –
KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII YA JINSIA WAZEE NA WATOTO. Muwakilishi wa bilal Tanzania ,mwakilishi wa
mstahiki meya wa kinondoni ,mama kairuki kutoka hospitali ya kairuki, diwani mama
Msofe kutoka kipunguni na wengine toka sehemu mbalimbali.
Mkurugenzi mtendaji wa Umoja wa wanawake wajane nchini Tanzania TAWIA Bi ROSE SARWAT akitoa maelezo mbele ya wakina mama hao |
Mgeni
rasmi mama SIHABA ambaye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo akizungumza
katika shughuli hiyo amesema kwamba serikali ipo makini na inamipango mingi
kuhusu wajane na kwamba wanajaribu kufanya marekebisho ya sheria kandamizi
zinazoweza kumkandamiza mwanamke mjane.pia alisema kuhusu kuwasaidia
anawashauri wanawake hao kuweza kujiunga kwenye vikundi mbalimbali vya mikopo
kuweza kijiinua kiuchumi..
Mgeni
toka umoja wa mataifa ambae ana asili ya kihindi amesema kuwa amefurahishwa kuona wajane wamekusanyika
pamoja na wanaweza kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili.huku akiisema
kuwa amefurahishwa na maneno ya mjane toka shinyanga ambaye aliyeweza kuishi na
hali hiyo ya ujane ndani ya miaka19 mpaka sasa, na ndugu wa mumewe waliweza
kuleta vizingiti vingi kwenye mali lakini alikuwa thabiti na kuweza kuvishinda
vizingiti hivyo hatimaye leo ameweza kupata haki yake,amesema kuwa umoja wa
mataifa uko sambamba na wajane wote duniani na kuhakikish wanapata haki zao
kupitia shirika lao linalo fuatlia haki za wajane duniani kote.pia amesisitiza
wahakikishe wanawapatia watoto wao elimu kwa maana ni funguo kwenye maisha yao
na ndio kitu pekee kitakachoweza kuwakomboa katika maisha yao.
Maadhimisho
hayo yalifanyika ndani ya uwanjua wa mnazi mmoja ambapo wanawake hao waliweza
kuweka kambi hapo huku wakipewa huduma mbalimbali zikiwemo za upimaji wa
magonjwa mbalimbali huduma iliyokuwa inasimamiwa na wataalam kutoka Hospitali
ya KAIRUKI
No comments:
Post a Comment