Thursday, June 30, 2016

SABASABA SPECIAL---TEMBELEA KOKOLIKO FASHION WAPO SABASABA KUKUPA BIDHAA BORA NA NZURI

 Aisha salim khoja ni miongoni mwawanawake wajasiriamali Tanzania ambae anatumia muda mwingi kujitangaza anawakaribisha watanzania wote kutembelea banda lake la KOKOLIKO  fashion linalipatikana ndani ya mabanda ya TWCC anabidhaa nyingi na nzuri anawakaribisha watanzania wote na wageni toka mataifa yote duniani kutembelea banda lake kuona bidhaa alizowaandalia.

Anamashati mazuri ya batiki vikapu vizuri alivyotengeneza kwa mikono yake.pia anapatikana Tanga unaweza kuwasiliana nae na popote africa anaweza kukuletea mzigo. 

Pia ukiacha shughuli hizi za kutengeneza mabatiki lakini pia anafanya kazi kama.kufundisha utengenezaji wa batiki na ujasilia mali kwa mabinti na wanawake wote, pia ni event organizer na anafanya fashion shows mbalimbali, pia yupo Tanga internatinal trade mark, na ni filamu producer.

Pia anasema kuwa changamoto anazokutana nazo ni upatikanaji wa masoko na anapenda kuwashauri tan trade wawe wanapanga mambo mapema na sio mpaka siku ya tukio ndo wanaanza kufuatilia vitu kama wafanya biashara wamechelewa kutoa vitambulisho imealazimu wao kulipa kama watu wengine wanao kuja kwenye maonyesho wakati wao ni wafanya biashara wa humo humo ndani.

No comments: