Tuesday, June 28, 2016

TGNP WAENDESHA WARSHA KWA VIONGOZI WA NGAZI YA JAMII NA JAMII KWA UJUMLA KUPEANA UZOEFU WA CHANGAMOTO WAKATI WA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YAO

Meneja wa idara ya maarifa na utafiti na uchambuzi GLORIA SECHAMBO akimwakilisha mkurugenzi mtendaji wa Mtandao wa jinsia Tanzania TGNP wakati akifungua warsha ya siku moja ya viongozi mbalimbali wa ngazi za jamii ambao ni mjuuisho wa madiwani,na viongozi wa vituo mbalimbali vya maarifa Jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja utekelezaji wa majukumu yaliyotokana na michakato mbalimbaliiliyofanyika katika jamii.

Wakati akizungumza alipokuwa anafungua mkutano huo amesema kuwa Kwa kufikiri zaidi jinsi ya kuweza kuwabana na kuwafanya viongozi wa jamii na wanajamii kwa ujumla walikuja na Bunge la jamii ambalo ni sehemu ya kuwapa nafasi wanajamii kukutana kuibua hoja zao na kuwafikishia viongozi wao na kuyafanyia maamuzi kwa pamoja njia ambayo amesema kuwa inasaidia sana kwa wanajamii kuwawajibisha viongozi wao na kudai uwajibikaji nchini ambapo warsaha hiyo imewakutanisha viongozi hao na wanajamii hasa wa maeneo ya kipunguni,mwananyamala na mabibo kupeana uzoefu tangu mfumo huo uanze.


Viongozi mbalimbali na wanaharakati waliokutanishwa kwa pamoja na TGNP ili kujadili maswala mbalimbali yakiwemo Elimu,Afya,Mapambano Dhidi ya ukatili wa jinsia ngazi ya jamii,ikiwa ni pamoja na kubainisha maswala ya uchechemuzi kupanga mikakati ya kuimarisha mapambano katika maendeleo ya maji,elimu na ukatili wa kijinsia.
Afisa Programe kutoka TGNP ANNA SANGAI akizngumza na wanajamii hao wakiwemo viongozi mbalimbali wa ngazi za jamii wakati wa Warsha hiyo iliyofanyika makao makuu ya ,mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Jijini Dar es salaam leo kwa lengo la kubadilishana uzoefu kuhusu kazi zao katika maeneo yao ya kila siku

No comments: