Kampuni ya Tigo Tanzania imetangaza ofa mpya ambayo watumiaji wote wa simu ambazo ni bandia watapata simu halisi kila watakapotembelea duka la huduma kwa wateja la Tigo kubadilishwa simu hizo.
Mradi huu unalenga kuwawezesha Watanzania kupata simu halisi kutokana na ukomo wa matumizi ya simu kwa wale walio na simu feki unafikia mwisho wake.
Mwanzoni mwa mwaka huu, Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitangaza kuwa simu zote bandia na ambazo sio za viwango vinavyokubalika ambazo ziko katika soko la Tanzania zitazimwa kuanzia Juni 16 mwaka huu.
Akitangaza ofa hiyo Mkuu wa Vifaa wa Tigo, David Zakaria alisema kuwa kampeni hiyo ya utambuzi imo katika mkakati wa kampuni katika kuisaidia mikakati ya serikali pamoja na Watanzania dhidi ya bidhaa bandia na hali kadhalika kukidhi usalama wa mifumo ya malipo ya Tigo Pesa.
Akifafanua kuhusu ofa hiyo kwamba kimsingi inawalenga wateja walio na simu bandia Zakaria alisema, “Tunawataka wateja wetu kutembelea maduka Tigo ya huduma kwa wateja yaliyopo nchi nzima kuhakiki simu zao na baada ya kuhakiki, wote wataobainika kuwa na simu feki watapata simu halisi aina ya Itel 2100 watakaponunua kifurushi cha 22,000/-.
Zakaria alisema ofa hiyo ni nono kwani kwa kawaida, simu hiyo huwa inauzwa kwa bei ya 30,000/- na sasa itapatikani kwa 22,000/- tu, huku akiongeza kuwa simu hiyo itakuwa na dakika 350 za kupiga simu bure katika mitandao yote, ujumbe wa maneno 1,000 na MB250 za intaneti kila mwezi kwa miezi mitatu.
No comments:
Post a Comment