Wednesday, June 1, 2016

UCHAGUZI YANGA UNASIMAMIWA NA TFF


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kuwafahgamisha wanachama wa Young Africans na familia ya mpira kwa ujumla kuwa mchakato wa uchaguzi wa Klabu ya Young Africans unaendelea vizuri na unasimaiwa na Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho kwa mujibu wa utaratibu ulioutoa awali.


Fomu za uchaguzi zinaendelea kuchukuliwa katika ofisi za Makao Makuu ya TFF-Karume. Vilevile fomu zinaweza kupatikana kwenye tovuti ya TFF amayo ni www.tff.or.tz.


TFF inafuatilia kwa karibu mwenendo mzima wa mchakato na taarifa zote zitatolewa na TFF kupitia wasemaji wake na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ambaye ni Wakili Msomi, Alloyce Komba.
Tayari Kamati ya Uchaguzi ya TFF, iliyopewa jukumu la kusimamia uchaguzi wa Klabu ya Young Africans imeridhishwa na mwenendo wa wanachama kwa namna wanavyochukua na kurejesha fomu.
Na kutokana na mipango yake, imesogeza mbele mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu mpaka Jumatatu Juni 6, 2016 saa 10:00 jioni.
Hadi sasa wanachama tisa (9) wamechukua na kurejesha fomu. Wanachama hao ni Aaron Nyanda na Titus Osoro wanaowania nafasi ya makamu mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 inayotambulika serikalini hadi sasa.
Wengine ni Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar. Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Juni 25, 2016.
Fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Vilevile utaratibu unafanyika ili fomu ziweze kupatikana katika tovuti ya shirikisho www.tff.or.tz
Fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000 kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti na Sh 100,000 kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji.  

No comments: