CHAMA cha ACT Wazalendo kinalaani vikali uamuzi wa jeshi la polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa uliotangazwa leo na Kamishna wa Polisi-Operesheni na Mafunzo Nsato M Msanzya-CP.
Ikumbukwe kuwa uamuzi huu wa jeshi la Polisi unafuatia kuzinduliwa kwa “Operesheni Linda Demokrasia” ya Chama cha ACT Wazalendo ili kumpa fursa Mbunge wetu Ndugu Zitto Kabwe na wabunge wengine wa upinzani waliosimamishwa Bungeni kuwaeleza kwa kina wananchi juu ya kuminywa kwa demokrasia kunakofanywa na uongozi wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania.
Mikutano ya “Operesheni Linda Demokrasia” inayoratibiwa na Chama chetu ilipangwa kufanyika kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya na Morogoro,mpaka sasa umeshafanyika mkutano mmoja jijini Dar esSalaam
Chama chetu kinapinga vikali uamuzi huu wa jeshi la polisi kwa sababu hauna mashiko.kwa kuwa haki ya vyama vya siasa kufanya mikutano ni ya kisheria kama ilivyoelezwa katika sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 kifungu cha 11(1) kamba “kila chama chenye usajiliwa muda au wa kudumu kina haki ya kufanya mikutano sehemu yoyote ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa ajili ya kujitangaza ”
Vile vile haki hiyo inalindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano ibara ya 18(1) juu ya uhuru wa kutoa maoni pamoja ibara ya 20(1) ya katiba hiyo hiyo juu ya uhuru wa kujikusanya
Jeshi la Polisi limeshindwa kuheshimu vipengele hivyo vya kisheria na kuamua kuzuia mikutano ya kisiasa
Sababu iliyotolewa na Jeshi la Polisi kuwa mikutano hii inalenga kuchochea wananchi kutotii sheria ni mwendelezo wa visingizio vya serikali vinavyolenga kuminya uhuru wa wananchi kuikosoa serikali na sasa Jeshi la Polisi limejiingiza katika kuisaidia serikali kutimiza matakwa yake ya ukandamizaji wa Demokrasia unaofanywa ndani na nje ya Bunge
Chama cha ACT-Wazalendo kinawasiliana na wanasheria wetu ili kupata tafsiri ya kimahakama ya uhalali wa jeshi la polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ambayo inatambuliwa na kulindwa na katiba.
Tunalikumbusha jeshi la polisi na serikali kwa ujumla kuwa hila hii ya kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani kamwe haitazuia nia njema tuliyonayo wala kushusha ari yetu ya kuitetea na kuilinda misingi ya demokrasia inapokandamizwa na serikali.
Ado Shaibu,
Katibu Itikadi, Mawasiliano na Uenezi
ACT Wazalendo
Baada ya Taarifa hiyo pia Taarifa Nyingine zinaeleza pia kuwa mikutano yote ya CHADEMA nayo ikapigwa Stop na Jeshi la Polisi kwa kile kilichoitwa Sababu za Kiinteligensia.Viongozi kadhaa wakatoa matamko yao.Unaweza kupitia hapa---
Niko Kahama polisi wamezuia mikutano yetu, nguvu kubwa imetumika na inatumika mpaka sasa kutawanya wananchi, nilidhani mtu anaejinasibu kuungwa mkono nchi nzima angejiamini kuliko yule asieungwa mkono,sasa ni wazi kwamba ndani ya serikali hii kuna madudu mengi sana na imejaa hofu tupu, walianza kwa kuweka bunge gizani hii yote ni kujaribu kuzuia taarifa zisiwafikie wananchi, sasa hata mikutano ya hadhara wanazuia eti kwasababu za kiintelijensia hivi hiyo intelijensia ya polisi iko kwenye mikutano ya Chadema tu? Haikuweza kutambua matukio makubwa ya ndugu zetu wanaouwawa kinyama kwa kuchinjwa?
#Hapa Hofu Tu
#Hapa Hofu Tu
Nimeshtushwa sana na uamuzi wa jeshi la polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Baada ya mafanikio makubwa ya mkutano wa kwanza wa hadhara jijini Dar Es salaam tangu uchaguzi Mkuu 2015 ilikuwa tuelekee Mwanza, Kigoma, Mpanda, Sumbawanga, Tunduma, Mbeya, Iringa na Morogoro. Polisi wameamua kuingia kwenye siasa kwa kuzuia Haki yetu ya kikatiba.
Chama cha ACT Wazalendo kitatoa kauli yake kuhusu suala hili ndani ya muda Mfupi. Hatutakubali unyemelezi wa udikteta nchini kwetu. Mungu yupo pamoja na wanaosimamia Haki
No comments:
Post a Comment