NA KAROLI VINSENT
Ni wazi kuwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu Juu nchini (HELB) ilikuwa inatafunwa kwa hiyo ni baada Wizara ya elimu,Sayansi na Teknolojia kubaini madudu mazito ndani ya Bodi hiyo.
Madudu hayo ni kuwepo kwa wanafunzi hewa ambao walikuwa wananufaika na mikopo hiyo pamoja na kuwepo wanafunzi ambao walikuwa wananufaika na mikopo hiyo kwa kulipwa na pande mbili yaani upande wa Bara HELSB pamoja na Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar (ZHESLB).
Sanjari na hayo pia Bodi hiyo imebainika kutumia Kampuni za Kidalali katika kuwadai wanafunzi mikopo huku ikiwa kinyume na taratibu za Bodi pamoja na Kampuni hizo kugubikwa na udanganyifu katika usajili wake kwenye orodha ya Makupuni nchini (BRELA).
Profesa Joyce Ndalichako ambaye ni Waziri Elimu,Sayansi na Teknolojia amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa anazungumza na Waandishi wa habari ambapo amesema baada ya terehe 16 February ya mwaka huu kuwasimaisha watendaji wa juu wa Bodi hiyo kutokana na kutokekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika taasisi hiyo pamoja na kupisha uchunguzi zaidi,
Ambapo Ukaguzi huo ulifanyika kwa kipindi maalum hadi march 2016 ,katika uchunguzi huo profesa Ndalichako amesema kumebainika kuwepo kwa wanafunzi hewa 50 ambao wamekuwa wakipata mkopo ambapo imeitia hasara serikali ya mamilioni ya fedha.
Amesema Uchunguzi huo pia umebaini zaidi ya wanafunzi 919 hewa ambao wanaelezwa kutoka chuo kikuu cha Dodoma ambao walikuwa wanapelekewa mikopo katika Chuo hicho ambapo kwa sasa imegundulikwa wanafunzi hawasomi chuo hicho ambao wameitia hasara serikali zaidi ya Bilioni Tatu.
Profesa Ndalichako amesema mbali na wanafunzi hao hewa pia Uchunguzi huo umebaini kuwepo kwa wanafunzi zaidi ya Laki moja ambao kisheria walikuwa wanatakiwa kuanza kulipa fedha walizokopeshwa na Bodi hiyo kutokana na kipindi cha mwaka mmoja kupita mara baada ya kumaliza chuo kama sheria inavyosema lakini amedai cha kushangaza wanafunzi hao bado hawajaanza kulipa mikopo hiyo.
Amesema licha kushindwa kukusanya Mikopo hiyo,Uchunguzi umebaini kuwa kuwepo na udhaifu mkubwa katika mfumo wa utunzaji taarifa za marejesho ya mikopo.
Amefafanua kuwa Kumbukumbu za HESLB zinaonyesha Madeni kwa kiwango pungufu kwa deni halisi huku akitoa mfano wanafunzi 262 walinufaika na mikopo kiasi cha SHS Bilioni 10 lakini amedai kuwa katika kumbukumbu za Bodi hiyo wanatakiwa kurejesha Bilioni 5.5 ambayo inakuwa pungufu ya karibia nusu ya deni ilo.
UFISADI KATIKA KAMPUNI ZA UDALALI ZILIPEWA TENDA YA KUFUATILIA WADAIWA.
Profesa Ndalichako pia amesema Uchunguzi huo umebainika kuwepo kwa utapeli anaoita wa “kitoto” kwa kampuni za udalali zilizopewa kufuatilia tenda.
“Iweje leo bodi ya mkopo iwakopeshe wanafunzi hao na kabla hata ya kutoa mikopo hiyo tayari ilichukua anuani zao,kuwafahamu wadhamini wao kwenye mikopo hiyo,pamoja na kujua wanapotoka lakini cha kushangaza wakati wa kudai fedha wanazitumia kampuni za udalali kudai fedha hizi”alishangaa Profesa Ndalichako.
Amesema Kampuni hizo zimebainika kuwepo na udanganyifu katika usajili wake huku akitaja jina Kampuni moja “Macho Mengi” ambayo haina hata usajili kwenye orodha ya Makampuni huku Kampuni mojawapo ikiwa imesajili Brela kwa kazi ya kufafirisha vifaa vya Jenzi jambo analodai inakuwa Kampuni ya Ujenzi inakuwaje leo ndio ipewa tenda ya kukusanya madeni ya mikopo.
Baada ya Madudu hayo,Waziri ameipa wiki mbili Bodi ya HESLB kuhakikisha wanawachukulia hatua kali za watumishi walihusika na ufisadi huo.
Ikiwemo kupitia Dosari zilizojitokeza pamoja na kuhakikisha wanavichukulia vyuo vikuu vilivyohusika kuwaruhusu wanafunzi kuchukua mikipo wakati wanasomavyo viwili tofauti
MADUDU YABAINIKA NACTE
Katika hatua nyingine Waziri huyo pia ameeleza madudu ya kutisha ndani ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kutokana na watendaji wake kushindwa kusimamia vyuo 567 vya ufundi vilivyopo chini yake kwa hatua ya kuwaruhusu wanafunzi “Vilaza” kujiunga na vyuo mbali mbali nchini.
Amesema Kamati Maalum iliyoundwa na yeye amesema imebaini pia kwa NACTE kuhusika hata katika kuwadahili watu wanasomea Shahada ya Kwanza (Bachelor) na Shahada ya Umahiri (Master) wakati sio jukumu lake lilopo kisheria.
Ameeleza kuwa ndani ya Bodi hiyo kumegundulika kuwepo kwa watumishi wasiokuwa na sifa.
“Leo inakuwaje mtu mwenye shahada moja anawasimia watu kama maprofesa huyu ataweza vipi”alihoji Profesa Ndalichako.
Profesa huyo amesema Nacte wameshindwa hata kuhakiki ubora wa vyuo vya kati nchini.
Hata hivyo,Profesa Ndalichako aliagiza Baraza hilo kutatua Changomoto hizo haraka sana.
No comments:
Post a Comment