Leo hii kamati ya haki,maadili na madaraka ya bunge leo inataraji kusoma taarifa ya shauri la Mbunge Joseph Mbilinyi baada ya kutoa ishara ya matusi bungeni na kunaswa na kamera za bunge!
Tunataraji Mbunge Mbilinyi kupewa adhabu kali ili iwe fundisho kwa vizazi na wabunge wa aina yake ndani na nje ya bunge!
Kwakuwa Joseph Mbilinyi alitoa ishara ya matusi kwa bunge na wabunge tulitegemea chama chake cha CHADEMA kingempa adhabu lakini wamenyamaza kimya!
Joseph Osmond Mbilinyi (Sugu) – Vikao 10
Joseph Mbilinyi (Mb) amekiri kunyoosha kidole cha kati juu wakati akitoka bungeni baada ya kusika mbunge amemtusi mama yake. Mh. Mbilinyi amejitetea kuwa ni kweli alinyoosha kidole cha kati juu baada ya kumsikia mbunge wa CCM akimtusi mama yake mzazi hivyo kupata short temper na kujikuta akitenda kosa hilo.
Pia Joseph Mbilinyi amesema kuwa alinyoosha kidole cha kati juu kama kupinga kile kilichokuwa kinafanyika na mbunge huyo wa CCM, alipoulizwa na Kamati ya Maadili inayoongozwa na Mh. Mkuchika, Mh. Mbilinyi alisema kuwa kunyoosha kidole cha kati juu hakina maana ya moja kwa moja hivyo kwa uelewa wake yeye alikuwa anapinga kitendo cha mbunge wa CCM.
Kamati ya maadili imeridhika kuwa kitendo cha Joseph Mbilinyi (Mb) kuonesha kidole cha kati juu ni kosa na kutoheshimu mamlaka ya Spika wa bunge baada ya kupitia matoleo ya maana mbalimbali ya (Kuonesha kidole cha kati juu) nchi tofauti tofauti.
Maazimio ya Kamati ya Maadili
Bunge limeazimia kuwa mbunge wa Mbeya Mh. Joseph Osmond Mbilinyi asimamishwe kuhudhuria vikao 10 vya bunge la 11 kuanzia kikao cha leo Juni 30 mpaka hapo adhabu itakapokuwa imekamilika. Bunge limepitisha kwa kauli moja adhabu hiyo.
Saed Kubenea – Vikao Vitano
Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea amepewa adhabu ya kutohudhuria bungeni vikao vitano mfululizo vya bunge la 11 kwa kosa la kutoa habari za uongo akiwa bungeni juu ya sakata la kiwanja cha Waziri wa Ulinzi Mheshimiwa Hussein Mwinyi kuwa ana mkataba wa kujenga nyumba za JWTZ
James ole Millya – Vikao vitano
Mbunge wa Simanjiro Mh. James Ole Millya amesimamishwa kutohudhuria vikao vitano vya Bunge kwa kosa la kusema uongo bungeni kuhusu Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu , sera ,bunge , kazi ,vijana , ajira na walemavu Jenista Mhagama kuwa na undugu na Yusuph Mhagama.
No comments:
Post a Comment