Sunday, June 12, 2016

WANAWAKE WA KANISA LA MORAVIAN MTONI KIJICHI KUFANYA MAOMBI MAKUBWA YA KUJIOMBEA NA TAIFA KWA UJUMLA

Wanawake wa Kanisa la Moravian Usharika wa Mtoni Kijichi wakiwa mbele ya kanisa lao Dar es Salaam leo asubuhi. Wanawake hao Julai 10 mwaka huu wanatarajia kufanya maombi ya kuwaombea wanawake wote nchini, familia zao pamoja na Taifa kwa ujumla.

Na Dotto Mwaibale

WANAWAKE wa Kanisa la Moravian Usharika wa Mtoni Kijichi wanarajia kufanya maombi makubwa kwa ajili ya wanawake nchini, familia zao pamoja na taifa kwa ujumla yenye lengo ya  kumshuru mwenyezi mungu.

Akizungumza na mtandao wa www. habari za jamii.com Mratibu wa tukio hilo Mwalimu Mary Anyitike alisema lengo la maombi hayo ambayo ni rami ni kumshukuru mungu kwa kuzaliwa wanawake.

Anyitke alisema maombi hayo yatafanyika katika kanisa hilo Julai 10, mwaka huu saa tatu asubuhi ambapo aliwaomba wanawake wote bila ya kujali dini na madhehebu yao kujitokeza kushiriki maombi hayo ambayo yapo kwa ajili yao.

"Maombi haya ni muhimu kwetu na familia zetu na kauli mbiu yetu ni wanawake ni jeshi kubwa" alisema Anyitike.

Aliongeza kuwa katika maombi hayo kutakuwa na sadaka ya kumskuru mungu pamoja na changizo la upatikana wa fedha za ujenzi wa kanisa hilo katika usharika huo.

No comments: