Tuesday, June 21, 2016

WAZIR MWAKYEMBE NAYE ALIJIA JUU GAZETI LA DIRA KWA UPOTOSHAJI

KYE1Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Waandishi wa Habari leo Mjini Dodoma kuhusu maadili ya Vyombo vya Habari katika kuhabarisha Umma juu ya miradi ya maendeleo na jinsi vinavyoweza kuwasidia wananchi kuleta maendeleo na kuepuka kutoa taarifa za upotoshaji.
KYE2Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe na Vyombo vya Habari leo Mjini Dodoma.


Na: Frank Mvungi – MAELEZO- Dodoma
Vyombo vya Habari  nchini Vimetakiwa kuzingatia weledi katika kutimiza majukumu yake ili kusaidia Taifa kufikia maendelo ya kweli na endelevu.
Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa mkutano na vyombo vya habari.
Akifafanua Mhe.  Mwakyembe amesema ili Taifa liwe na Maendeleo ni lazima kuwa na Vyombo vya Habari vinavyozingatia weledi wa taaluma ya uandishi wa habari pamoja na Sheria na Kanuni zinazosimamia tasnia hiyo.
“Navipongeza Vyombo vingi vya Habari hapa nchini ambavyo vinafanya kazi nzuri ya kuelemisha Umma na kuchochea maendeleo ya nchi yetu ila kuna wachache ambao kwa makusudi wameamua kupotosha Umma” alisisistiza Dkt. Mwakyembe
Hivi Karibuni gazeti moja lilitoa taarifa zinapotosha Umma kwa kumhusisha Waziri huyo na maswala ya Ufisadi ambapo alitumia fursa hiyo kuviasa vyombo vya habari kuepuka kuandika au kusambaza habari ambazo ni za upotoshaji na hazina maslahi kwa Taifa na hazijafanyiwa uchunguzi wa kina.
Akitolea mfano chombo hicho cha habari Mwakyembe amesema kuwa, kimekuwa kikiripoti taarifa zinazogusa masuaa ya Ulinzi na Usalama pasipo kuangalia maslahi ya Taifa kwanza hali inayoonyesha kukosekana kwa uzalendo.
Mwakyembe aliongeza kuwa tasnia ya habari imekuwa na ni vema sasa waandishi wote kuzingatia maadili ya taaluma hiyo ili kuepuka kufikishwa katika vyombo vya sheria  kwa kukiuka sheria na kanuni za uandishi wa habari.
Tasnia ya Habari ni muhimili muhimu katika kuchochea Maendelo ya Taifa lolote lile kwa kuelimisha kuhamasisha na kuamsha ari ya wananchi kujiletea maendeleo.

No comments: