Katika hotuba yake amemupongeza Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ali kwa juhudi zake za kuwaunganisha waislamu wote na kupanua wigo wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kutoa huduma za kijamii na ameahidi kuwa serikali ya awamu ya tano itaunga mkono juhudi hizo.
Rais Magufuli amesema kitendo cha kuwaunganisha waislamu wote katika Baraza la Eid el-Fitr kinafungua ukurasa mpya na ni moja ya hatua muhimu za kuimarisha amani, umoja na mshikamano miongoni mwa waislamu wa makundi mbalimbali pamoja na watanzania wengine waisio waislamu.
Aidha Rais Magufuli amezungumzia juhudi zinazofanywa na BAKWATA katika kuimarisha taasisi zake zinazotoa huduma za kijamii na kulinda mali zake akisema serikali itahakikisha mali zote za waislamu zinakuwa salama na kwamba wote waliodhulumu mali za waislamu watazirejesha.
No comments:
Post a Comment