Meneja wa Milvik Tanzania,Tom Chaplin (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Tigo Kijitonyama Dar es Salaam leo asubuhi, wakati akitangaza ushirikiano kati yao na Tigo kutoa bima watakayoimudu watanzania. Kutoka kushoto ni Meneja wa Promosheni wa Tigo, Mary Rutta, Mkuu wa Huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel na Meneja Maendeleo ya Biashara wa Resolution Insurance, Zamaradi Mbega.
Mkuu wa Huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel (wa pili kulia), akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja wa Promosheni wa Tigo, Mary Rutta akitoa ufafanuzi mbalimbali kuhusu bima hiyo.
Meneja Maendeleo ya Biashara wa Resolution Insurance, Zamaradi Mbega (kulia), akizungumzia mpango huo wa bima.
KAMPUNI ya Simu ya Tigo Tanzania itashirikiana na na Milviki Tanzania na kampuni ya bima ya Resolution kuanzisha huduma mpaya ya Bima iliyoboreshwa ikijulikana Bima Mkononi. Tigo imekuwa ikitoa huduma kama hiyo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa wateja wake zaidi ya 500,000 kupitia Tigo Bima.Huduma ya Bima Mkononi inatoka huduma ya kipekee kama vile bima ya maisha, ugonjwana ajali kwa mtu binafsi kwawateja ambao wanaotumia huduma ya Tigo Pesa.
Akitangaza kuzinduliwa kwa huduma hiyo jijini Dar es Salaam leo Meneja wa Milvik Tanzania,Tom Chaplin alisema, “Huduma hii itasaidia kuziba pengo kati ya wateja na hivyo kuongeza upenyezaji wa huduma hiyo kwa njia ya simu katika maeneo ya mjini na vijijini nchini Tanzania, tunaamini Bima Mkononi itakuwa ni kicdhocheo kikubwa cha kusukuma ujumuishwaji wa huduma za fedha katika sekta isiyo rasmi kwa kuwawezesha Watanzania kuzifikia huduma za bima wanazozimudu kutoka kwenye simu zao.”
Chaplain aliongeza, “Tunawaomba Watanzania ambao hawajaweza kuzifikia huduma za afya ambao wanazimudu ao bima ya kawaida ya afya kuanza kutumia huduma hii kwa sababu inatoa ulinzi dhidi ya majanga ya kifedha na afya duni kwao na familia zao.”
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Huduma za kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel alisema, “Kuzinduliwa kwa huduma hii kupo kwenye mikakati ya Tigo ya kuboresha mageuzo katika mfumo wa maisha ya kidijitali na katika kuongoza kwake katika kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu kwa kuwezesha huduma ya Bima Mkononi kufikiwa kupitia Tigo Pesa.”
Aliongeza, “Huduma hii mpya itakuwa ni fursa kubwa kwa wateja wa Tigo kuipata huduma ya bima kwa urahisi kwa sababu huduma ya Bima Mkononi inalenga kuwapatia Watanzania njia mbadala kwa bima za afya na maisha.”
Aliipongeza Milvik kwa ushirikiano wake na kuahidi kuwa Tigo imelenga kuendelsa kuunga mkono kupitia huduma ya Tigo Pesa.
Hivi karibuni Tigo ilizindua kampeni mpya ya NITIGOPESA ambapo wateja kutoka mitandao yote ya simu wanaweza kupata huduma za kifedha kutoka kwa wateja na wafanyabiashara kote nchini.
No comments:
Post a Comment