……………………………………………………………………………………………………
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
DAR ES SALAAM
Kanali mstaafu na mchambuzi wa masuala ya Habari na jamii Dkt Haruni Kondo amewaasa watanzania kuchukua tahadhari na watu wenye uroho wa fedha na madaraka kwa kuwaaminisha wananchi kuwa maandamano na vurugu ndio demokkrasia na ukombozi wa umaskini wetu.
Kanali Kondo alisema kuwa watu wa aina hiyo ni wakuogopwa kama ukoma kwani ni hatari kwa ustawi na maendeleo ya nchi yetu ambapo tunashuhudia vurugu, vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi mbalimbali duniani na madhara yake.
“watanzania tuchukue taadhari ya watu wenye uroho wa fedha na madaraka kwani kumekuwa na watu wanaotuhamasisha ya kuwa maandamano na vurugu ndiyo ukombozi wa umaskini wetu hivyo tunapaswa kuchukua taadhari na kukataa hadaa hizo” alisema Kanali Kondo.
Vilevile aliongeza kuwa, roho mbaya imechangia taifa letu kudumaa kimaendeleo kutokana na ubinafsi wa baadhi ya viongozi wetu wakiwemo wanasiasa, wafanyabiashara, watumishi wa umma, wasomi na wananchi wa kawaida.
Aidha,alifafanua kuwa katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais John Pombe Magufuli amechukua hatua ngumu ya kupambana na vitendo vya rushwa, ubadhilifu na ufisadi kwani kitendo hicho kimewaudhi mafisadi na mawakala wanaopotosha ukweli na kuendesha propaganda chafu dhidi ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano.
No comments:
Post a Comment