Na Exaud Mtei
Wakati bunge la bajeti
la Tanzania likimalizika Mjini Dodoma na kushughudia bajeti ikipitishwa
hatimaye Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania LHRC kimetoa
tathmini yake juu ya bunge hilo huku ikionyesha baadhi ya kasoro ambazo
zilijitokeza huku wakiutaka uongozi wa bunge kuzifanyia kazi kwani zimetia doa
shughuli za bunge hilo.
Bunge la mwaka huu
limemalizika huku kukiwa na msuguano mkali wa kisiasa na kiuongozi ambapo hadi
mwisho wa bunge hilo ulishughudiwa wabunge wa vyama vya upinzani wakisusa
kushiriki katika vikao vyake kwa kile walichokiita kutokuwa na Imani na Naibu
Spika wa bunge hilo Mh TULIA AKSON.
Akizungumza na
wanahabari leo Jijini Dar es salaam Kaimu mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za
binadamu nchini Tanzania LHRC Bi IMELDA LULU URIO ametaja baadhi ya mambo
ambayo wao kama wafwatiliaji wa shughuli za bunge hilo yalitia doa katika
uendeshaji wa bunge hilo.
Akitaja baadhi ya mambo
hayo amesema kuwa swala la haki ya kupata habari lilikuwa ni changamoto kubwa kwa
bunge hilo kutokana na kwa mara ya kwanza serikali kusitisha urushwaji wa
matangazo ya bunge Live kwa kile walichokiita kubana matumizi jambo ambalo
amesema kuwa limekuwa ni moja ya kikwazo kikubwa cha wananchi kupata habari huku
akiishauri serikali kufikiria upya swala hilo ili kuhakikisha kuwa wananchi
wanapata nafasi ya kupata habari kwa uhuru na uhakika kama ilivyokuwa awali.
Amesema kuwa katika
bunge la bajeti pamoja na serikali kuanzisha mfumo mpya wa kurusha matangazo
hayo kwa kuyarekodi na kuyarusha wakati wa usiku bado nafasi hiyo sio Rafiki
kwa wananchi walio wengi kwani muda wa usiku wananchi wengi wanakuwa hawapati
nafasi ya kusikiliza na kuangalia vipindi hivyo huku akiongeza kuwa sio jukumu
la bunge kurusha matangazo hiyo ni kazi ya vyombo vya habari na bunge kazi yake
ni kuishauri na kuikosoa serikali.
IMELDA ametaja kasoro
nyingine ambazo zilionekana katika bunge hilo ni swala la wabunge kutotimiza
wajibu wao kwa wananchi,ambapo katika bunge hilo imeonekana wazi kuwa wabunge
wengi hasa wa chama tawala wamekuwa wakitetea sana maslahi ya chama chao na
kusahau kabisa maslahi ya nchi na kuibua hoja za kuisaidia jamii kwa ujumla.
Amesema pia swala la
wabunge wa vyama vya upinzani kugomea vikao vya bunge kwa kipindi chote cha
mjadala wa bajeti na kusababisha bajeti ya Tanzania kupitishwa na wabunge 252
kati ya wabunge wa 384 kumewanyima wananchi
haki ya uwakilishwa na wawakilishi wao waliowachagua.
Wanahabari mbalimbali wakifwatilia mkutano huo |
Mambo mangine ambayo
yametajwa kama kasoro katika bunge hilo ni pamoja na kukosekana kwa umoja wa bunge
kama muhimili,kukosekana heshima na kuheshimiana baina ya wabunge ambapo
mijadala mingi ilitawaliwa na vijembe,matusi na kukashifiana ambapo maswala
hayo yamekuwa yakiwaudhi wananchi.
Kukiukwa kwa kanuni za
bunge na matumizi mabaya ya muda wakati wa uchangiaji nazo zimetajwa kama
changamoto kubwa katika bunge hilo
ambapo kwa mujibu wa kanuni za bunge mbunge ataweza kuchangia mwisho ni
muda wa dakika 60 laini katika bunge hilo ilishighudiwa wabunge wakizidisha
muda lakini kumekuwa hakuna hatua zilizochukuliwa.
Katika hatua nyingine
LHRC wameutaka uongozi wa bunge kupitia kwa spika na Naibu Spika kuhakikisha
kuwa wanatatua migogoro iliyowagawa wabunge kwa njia ya Amani huku
wakihakikisha kuwa sheria na kanuni za bunge zinafwatwa na wabunge wote wa
Tanzania.
No comments:
Post a Comment