Sunday, July 3, 2016

MBUNGE WA NDANDA AENDELEA KUTIMIZA AHADI ZAKE KWA WALIOMCHAGUA,HII NI MPYA KUTOKA KWAKE

Diwani wa kata ya ndanda Costansia Ng’ombo  akimkabidhi saruji mtendaji wa kijiji cha mpowora ndug THABIT CHINDEMA  kwa ajili ya ujenzi wa choo cha shule



Mbunge wa jimbo la Ndanda,mkoani Mtwara, Cecil Mwambe amekabidhi saruji ipatayo tani 65 katika kata mbalimbali jimboni humo kwa lengo la kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa ahadi alizotoa wakati wa kampeni.

Akizungumza juzi na jana wakati wa kukabidhi saruji hiyo katika maeneo yaliyokusudiwa alisema kuwa amefikia maamuzi hayo kutokana na hali mbaya alizokutana nazo katika maeneo mbalimbali wakati kampeni hivyo hana budi kutekeleza alichoahidi.

“Wakati wa kampeni nilikuja kwa wananchi hawa kuomba kura,kwa macho yangu niliweza kujionea hali halisi namna wananvyokabiliwa na changamoto mbalimbali kama ukosefu wa zahanati na vyumba vya madara na sasa nimeweza kutekeleza ahadi yangu hivyo niombe wananchi nao wajitolee nguvu kazi ili kuweza kuibadilisha Ndanda yetu,”alisema Mwambe

Akizungumza Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mraushi kata ya Lukuledi,Modesta Charles ambao ni wanufaika wa saruji hiyo alisema itawawezesha kujenga vyumba vya madarasa na wanafunzi kuondokana na hatari ya kuangukiwa na vymba vilivyo chakavu.

“Tunakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madarasa na matundu ya vyoo lakini wananchi tayari walishajitolewa kusomba mchanga wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na leo mbunge ametimiza ahadi yake ya saruji,hii ni faraja kwasababu watoto wanasoma katika mazingira magumu na kwa hofu ya kuangukiwa na ukuta kwasababu ni chakavu na ni ya udongo na walikuwa wanachafuka sana na ukiangalia kijiji chote tunakabiliwa na tatizo la maji,”alisema mwalimu Charles.

Akizungumza diwani wa kata ya Mlingula,Jackson Kusanda kwa niaba ya wananchi baada ya kupokea saruji kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na choo alishukuru kwa msaada huo na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano.

“Namshukuru mbunge kwa mchango huu kwa niaba ya wananchi,hivyo niwaombe watoe ushirikiano ili kukamilisha kile tulichokusudia,’alisema Kusanda

Naye diwani wa kata Ndanda,Costansia Ng’ombo wakati wa kukabidhiwa saruji kwaajili ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mpowora alisema wanafunzi walikuwa wakikabiliwa na tatizo la vyoohivyo saruji hiyo itawawezesha kuondokana na tatizo hilo.

Sehemu ya saruji hiyo pia itatumika katika kufyatua tofauli kwaajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Chiroro kata ya Namajani.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chwata kata ya Chiwata Rajabu mndamba akipokea saruji kwa ajili ya ujenzi wa Darasa la awali toka kwa Dada Zaida kwa niaba ya mbunge wa jimbo la Ndanda CECIL MWAMBE
Akizungumza Getruda Msofe ambaye ni Mtendaji wa kata ya Namajani alisema kuwa kupatikana kwa saruji hiyo kutawezesha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Chiroro kata ya Namajani kwasababu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya zahanati na kulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hasa wakina mama wajawazito na watoto.

Naye Zainabu Mrope alisema kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hiyo kutawasaidia kupata huduma za afya ya mama na mtoto kwa wakati.

"Tunashukuru Kwa mchango wa mbunge kwasababu zahanati itakapokamilika itatusaidia kupata huduma kwa karibu kwasababu hasa sisi kina mama tumekuwa tukitembea umbali mrefu siku za kuhudhuria kliniki na wakati mwingine wenzetu kwa bahati mbaya walikuwa wakijifungulia njiani,"alisema Zainabu
Mbunge wa Jimbo la ndanda CECIL MWAMBE akiangalia baadhi ya matofali yaliyofwatuliwa kwa nguvu za wananchi kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya ya kijiji cha Chiroro kata ya Namajani
Vijana wakishusha Saruji hiyo kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya msingi Mraushi iliyotolewa na mbunge huyo
Mbunge wa Jimbo la ndanda CECIL MWAMBE akizngumza na wanawake wa kijiji cha 

No comments: