Msanii Abino aliyevaa T-shit nyeupe akizungumza moja kwa moja kutoka Radio TBC FM katika kipindi cha NDIO MAMBO wakati wa mahojiano yake leo |
Na Exaud Mtei
Msanii wa muziki wa Hip
Hop Tanzania anayechipukia kwa kasi GOOD MANSON maarufu kwa jina la ALBINO leo
amepata nafasi ya kueleza maswala mbalimbali yanayohusu mziki wake na harakati
za kuukuza kitaifa na kimataifa Zaidi ndani
ya Radio TBC FM katika kipindi cha NDIO MAMBO kinachoongozwa na watangazaji BK
na JCLK.
Akizungumza katika
kipindi hiko kilichorushwa na Radio TBC FM amesema kwa sasa amekwisha Rekodi
nyimbo 16 kwa mfumo wa Audio katika studio mbalimbali nyingi zikiwa za mkoani
arusha na moshi ambapo amesema kwa sasa ameamua kuja Jijini Dar es salaam ili
kupanua mziki wake Zaidi baada ya kuona Dar es salaam ni mkoa ambao unaweza
kumpa mafanikio Zaidi kimuziki.
Msanii huyo ambaye
anatamba na nyimbo yake mpya ya Rafiki yangu hela amesema kuwa katika harakati
zake za kufanya muziki amekuwa akikutana na changamoto kubwa zikiwemo pia za
kuweza kuwapata waandaaji wazuri wa muziki kipindi ambacho alikuwa nje ya Dar
es salaam lakini kwa sasa amekuja Dar es salaam kwa ajili ya kufanya muziki
hivyo akawataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwani kazi nzuri zinakuja
ikiwemo Video ya Nyimbo yake mpya ya Rafiki yangu hela.
Akizungumzia nyimbo
hiyo yake mpya amesema kuwa Wimbo wa Rafiki yangu hela ameimba kutokana na
ukweli kuwa katika maisha ya sasa kila kitu kinahitaji hela hivyo ni ukweli usiopigika
kuwa katika marafiki wazuri duniani hela nayo ipo hivyo ameimba ili kuwakumbusha
watanzania na vijana kutafuta hela kwa nguvu na Hari kubwa ambapo wimbo huo upo
katika hatua za mwisho kufanyiwa video na kampuni ya NORTWOOD MEDIA ya mkoani
chini ya THK.
Aidha akieleza mipango yake ya kufanya colabo na wasanii mbalimbali wa ndani ya Tanzania wanaofanya vizuri amesema kuwa kwa sasa mipango yake ni kufanya ngoma na msanii Benpol na linex na mipango hiyo inaendelea vizuri huku akisema anahitaji kufanya kazi na wasanii wengine Zaidi kwa kuwa mziki sasa ni biashara na sio kujifurahisha kama ilivyodhaniwa na wengi.
KUSIKILIZA WIMBO WA HELA WA MSANII ALBINO NIMEKUWEKEA CHINI HAPO
No comments:
Post a Comment