Tuesday, July 5, 2016

PBZ Yakabidhi Msaada kwa Watoto Wa Vituo Vya Mayatima Zanzibar Kusherehekea Sikuku ya Eid Fitry


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg. Juma Ameir akizungumza na wakati wa kukabidhi msaada wa Vyakula kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar, ili kusherehekea Sikukuu baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hafla hiyo ya makabidhiano ilifanyika katika Nyumba ya Watoto Mazizini Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) akikabidhi msaada wa vyakula kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar kusherehekea vizuri sikuku ya Eid Fitry baada ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuungana na Watoto wenzao kusherehekea sikuku hiyo. 
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akisalimiana na Watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar alipowasili kwa ajili ya kukabidhi misaada ya Vyakula kwa Watoto hao kusherehekea Sikukuu ya Eid Firty.  
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akisalimiana na Watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar alipowasili kwa ajili ya kukabidhi misaada ya Vyakula kwa Watoto hao kusherehekea Sikukuu ya Eid Firty.  
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Ndg. Juma Ameir akizungumzac wakati wa kukabidhi msaada wa Vyakula kwa Watoto wa Kijiji cha SOS Zanzibar.kushoto baaddhi ya watoto wa kijiji hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa PBZ Ndg Juma Ameir akiwakabidhi msaada wa Vyakula Watoto wa Kijiji cha SOS Zanzibar ili kusherehekea vizuri Sikukuu ya Eid Fitry baada ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kijiji hicho huko mombasa Zanzibar. 
Watoto wa Kijiji cha SOS Zanzibar wakimsikiliza Mtoto mwezao akitowa neno la shukrani kwa Uongozi wa PBZ kwa msaada wao huo. 
Mtoto wa Kijiji cha SOS Zanzibar akitowa neno la shukrani kwa Uongozi wa PBZ kwa msaada wao huo.
Afisa Masoko wa PBZ Ndg Mohammed Nuhu akiwa na Mlezi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Islah Center Bi Zalha Abdalla 
Afisa Masoko wa PBZ Ndg Mohammed Nuhu akitowa maelezo kwa Watoto wa Kituo cha Watoto Yatima cha Islah Center kilichoko mombasa Zanzibar kulia Mlezi Mkuu wa Kituo hicho Bi Zalha Abdalla 
Watoto wa Kituo cha Watoto Yatima cha Islah Center cha Mombasa Zanzibar wakisoma dua kuwaombea Wafanyakazi wa PBZ na Uongozi wao kwa msaada wao huo na kutowa shukrani.
Imetayarishwa na OthmanMapara 
Zanzinews,Blogspot.Com
Email othmanmaulid@gmail.com

No comments: