Wednesday, July 13, 2016

RAIS AVIAGIZA VYOMBO VYA USALAMA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA WAKATI

DAW1Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimuonesha Rais Dkt. John Pombe Magufuli sehemu ya Madawati yaliyotengenezwa na fedha zilizopatikana kutokana na kubana matumizi kutoka Ofisi ya Bunge katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
DAW2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua Madawati hayo yaliyotengenezwa na Jeshi la Magereza pamoja na Suma JKT.
DAW4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amekaa kwenye moja ya Dawati katika hafla hiyo fupi ya ugawaji wa Madawati hayo.
DAW5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya Msingi Bunge George Samwel wakati akiangalia mfano wa darasa ya jinsi madawati hayo yatakavyo katika katika shule mbalimbali nchini.
DAW7Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya Msingi Bunge George Samwel akimtajia Mheshimiwa Rais Jina la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumuuliza huku Waziri Mkuu akitazama kwa furaha.
DAW8Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu ambaye aliyapokea kwa niaba ya Wabunge wa majimbo mbalimbali nchini.
DAW9Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ndogo ya Tume ya huduma za Bunge inayoshughulika utengenezaji wa madawati. Waliosimama mbele ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu pamoja na Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi.
DAW10Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya msingi Bunge mara baada ya tukio la kukabidhi madawati katika Majimbo mbalimbali nchini. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson pamoja na Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako.
DAW11Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya Maaskari brass bendi ya Jeshi la Magereza mara baada ya kukabidhi Madawati.
DAW12Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
DAW13Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwanafunzi wa Darasa la tatu katika Shule ya Msingi Bunge Mariam Samwel wakati akiondoka kwenye viwanja hivyo.
DAW14Sehemu ya Madawati yaliyokabidhiwa leo.
DAW15Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyehudhuria hafla hiyo ya ugawaji wa Madawati katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

………………………………………………………………………………………………..
Na: Lilian Lundo – Maelezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameviagiza vyombo vya Usalama vilivyopewa jukumu la kutengeneza madawati kujipanga zaidi ili kutekeleza kwa wakati majukumu wanayopewa.
Mhe. Rais aliitoa kauli hiyo leo, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya uzinduzi wa mpango wa ugawaji wa madawati yaliyotolewa na Ofisi ya Bunge kwa Majimbo 155 ikiwa ni awamu ya kwanza ya ugawaji wa madawati hayo.
Mnamo april 11, 2016 Mhe. Rais alipokea hundi ya shilingi Bilioni Sita kutoka Ofisi ya Bunge na kuagiza fedha hizo zielekezwe katika utekelezaji wa utengenezaji wa madawati ambapo Magereza na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) walipewa jukumu la kutengeneza madawati hayo.
Aidha Mhe. Rais amesikitishwa na kasi ambayo JKT na Magereza wametumia katika utengenezaji wa madawati hayo, ambapo kwa miezi mitatu wametengeneza jumla ya  madawati elfu Sitini.
“Nina wasiwasi na kasi yenu, ikiwa kwa miezi mitatu mmetengeneza madawati elfu sitini basi kuna uwezekano wa zoezi hili la utengenezaji wa madawati mkamaliza mwaka 2017,” alifafanua Mhe. Rais.
Aliendelea kwa kusema kuwa, suala la madawati ni la haraka alihitaji kusubiri kwa muda mrefu hivyo vyombo hivyo vinatakiwa kutengeneza madawati hayo kwa uharaka kwani nguvu kazi ya kutosha wanayo.
Kwa upande wake, Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson amesema kuwa Ofisi ya Bunge inategemea kugawa madawati 120,000 kwa awamu mbili tofauti ambapo awamu ya kwanza imekamilika na jumla ya madawati 61,385 yatagawiwa kwa majimbo 155 kati ya majimbo 264. 
Fedha iliyotolewa na Ofisi ya Bunge ni Fedha iliyotokana na matunda ya  mpango wa Serikali wa kubana matumizi ambapo Ofisi ya Bunge imeweza kubana matumizi na kubaki na Shilingi Bilioni Sita kwa mwaka wa fedha 2015/2016.

No comments: