Zaidi ya madiwani 20
kutoka katika kata mbalimbali nchini Tanzania leo wameanza kupatiwa mafunzo ya
siku tano yakiwa na lengo la kuwaongezea uelewa kuhusu dhana ya bajeti kwa
,mlengo wa kijinsia na matumizi yake katika kutengeneza mipango na bajeti
kupitia nafasi walizo nazo.
Mafunzo hayo maalum
yamefanyika Jijini Dar es salaam ambayo yameandaliwa na mtandao wa jinsia
nchini Tanzania TGNP na kuwakutanisha madiwani kutoka katika kata tofauti hapa
nchini ambapo yamegfunguliwa Rasmi na Mkurugenzi wa Mtandao huo LILIAN LIUNDI.
Akifungua mafunzo hayo
Liliani Liundi amesema kuwa lengo la TGNP ni kufwatilia na kunoa uelewa wa
viongozi hao kuhusu maswala mazima ya bajeti ikiwa ni pamoja na kufwatilia jinsi
bajeti inavyotoka na kutumika hususani bajeti yenye mlengo wa kijinsia ambayo
amesema ni bajeti ambayo inapanga Rasilimali kulingana na makundi mbalimbali
yaliyopo katika jamii zetu alkisisitiza kuwa itakuwa ni bajeti ya haki kwa wananchi wote.
Amesema kuwa mafunzo
hayo yamelenga kuwawezesha viongozi hao kutambua haki mbalimbali za makundi
katika jamii katika Bajeti ya Tanzania na kuwajengea uwezo mkubwa wa kiuongozi
hususani kuitumia Bajeti hiyo katika kuwasaidia wananchi hususani makundi yaliyopo katika jamii zao.
Baadhi ya waheshimiwa madiwani kutoka kata mbalimbali za Tanzania wakiwa wanasikiliza kwa makini mafunzo hayo ambayo yatadumu kwa siku Tano ndani ya mtandao wa TGNP Dar es salaam |
Baadhi ya madiwani
ambao wamezngumza na mtandao huu juu ya mafunzo hayo wamesema kuwa mafunzo hayo
yamekuja katika wakati muafaka ambao bajeti ya Tanzania imesomwa na sasa ni
kazi ya viongozi wa ngazi za chini ambao ndio wanaokwenda kuitumia bajeti hiyo hivyo
wameshukuru sana waanzilishi wa mafunzo hayo kwa kuwa yatawasaidia katika
utendaji wao wa kazi kila siku.
No comments:
Post a Comment