Thursday, July 28, 2016

UTAFITI--ASILIMIA 80 YA WANAHABARI NCHINI TANZANIA NI VIBARUA YABAINIKA HAWANA MIKATABA KAZINI


Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo ALFRED MAPUNDA kutoka Wizara ya Viwanda na biiashara akiwaongoza viongozi wa LHRC kuzindua Rasmi Report ya haki za binadamu katika biashara ya mwaka 2015 Leo Jijini Dar es salaam

 Exaud Mtei-- Dar es salaam

Wakati wanahabari wakitajwa kama ni mhimili wanne wa nchi yoyote duniani ncini Tanzania utafiti umeonyesha kuwa asilimia 80 ya wanahabari waliopo katika maoifisi mbalimbali hawana mikataba ya kazi na wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea kama vibarua jambo ambalo limetajwa kuwa ni hatari kwa ustawi wa tasnia hiyo muhimu katika taifa lolote.

Hayo yamebainika leo Jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa Report maalum ya haki za binadamu katika biashara ambayo imetolewa na kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania LHRC Report ambayo huwa inaonyesha maeneo mbalimbali ambayo haki za binadamu zinakiukwa hususani katika maeneo ya kazi zikiwemo kampuni,masokoni,mashambani na maeneo mengine mengi.
Report hiyo ambayo imezinduliwa na Mwakilishi kutoka wizara ya viwanda na Biashara Mh ALFRED MAPUNDA ambaye ni kaimu mkurugenzi wa sera na wizara ya viwanda na biashara imeonyesha kuwa Asilimia Zaidi ya 60 ya wafanyakazi nchini wanafanya kazi bila mikataba inayoeleweka huku kundi la wanahabari na wabeba mizigo maarufu kama potters wakitajwa kuwepo katika idadi hiyo.

Mtafiti wa Report Hiyo kutoka LHRC Bwana Clarence Kipobota akisisitiza yaliyomo katika Report Hiyo
Akitoa maelezo kadhaa kuhusu utafiti huo Mtafiti wa Report Hiyo kutoka LHRC Bwana Clarence Kipobota amesema kuwa utafiti huo umefanyika Takribani mikoa 16 nchini Tanzania na kwa njia mbalimbali zikiwemo kuwatembelea watanzania katika maeneo yao ya kazi na kuzungumza nao na kujua maswala mbalimbali yanayowakabili yakiwemo hayo ya mikataba kazini na wafanyakazi Zaidi ya mia saba walifikiwa na Utafiti huo

Amesema kuwa idadi hiyo ya wafanyakazi ambao hawana mikataba ni kubwa kiasi ambacho kinaweza kuikosesha serikali mapato makubwa kuwa kuwa ili mfanyakazi afanye kazi na kulipa kodi halali inapaswa awe na mkataba imara ambao unamwonuesha kuwa yeye ni mfanyakazi halali wa sememu husika tofauti na sasa ambapo wengi wanafanya kazi kama vibaria
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Report hiyo Mkurugenzi wa kituo hicho cha LHRC Mama HELLEN KIJO BISIMBA amesema kuwa sababu kubwa inayowafanya baadhi ya wafanyakazi wakiwemo wanahabari kufanya kazi bila mikataba ni kushindwa kuunda vyama vyao vya umoja vya kuwatetea katika maswala hayo jambo ambalo amesema limewasaidia wafanyakazi wengine wakiwemo madereva ambao kwa sasa wana umoja wao na wanaweza kusimama kudai haki zao.

Amewashauri wanahabari nchini Tanzania kuhakikisha kuwa pamoja na kufanya kazi kubwa ya kuwatetea watanzania walio wengi ni wakati sasa na wao kuwa na umoja wao wa wafanya kazi ili waweze kupata msaada mbalimbali wa kimaslahi kutoka kwa wahusika waliowaajiri.

Aidha mgeni Rasmi katika uzinduzi kutoka wizara ya viwanda na Biashara Mh ALFRED MAPUNDA ambaye ni kaimu mkurugenzi wa sera na wizara ya viwanda na biashara amekipongeza kituo hicho kwa kuendeleza kutoa Taarifa hizo ambazo zimekuwa zikitumika na serikali kwa kiwango kikubwa katika kufanya mabadiliko katika maeneo mbalimbali hususani katika meneo ya ajira na biashara kwa ujumla
Picha Ya pamoja

No comments: