Na Exaud Mtei
Wakati serikali ya
awamu ya Tano nchini Tanzania ikiendelea na uteuzi wa nafasi mbalimbali za
utumishi serikalini zikiwemo zile za wakurugenzi,wakuu wa wilaya na watumishi
wengine hatimaye hoja ya kupungua kwa uteuzi wa wanawake katika nafasi hizo
imeanza kuibua mijadala mbalimbali huku baadhi ya wanaharakati wakitoka
hadharani na kukosoa uteuzi huo waliosema unarudisha nyuma harakati za kuleta
usawa wa kijinsia.
Wiki moja iliyopota
Rais wa Jumhuri ya muungano wa Tanzania DR JOHN MAGUFULI alifanya uteuzi wa
nafasi za wakurugenzi wa wilaya na mikoa mbalimbali huku katika uteuzi huo
ikionyesha kushuka kwa ushirikishwaji wa wanawake jambo ambalo limeanza kuzua minongono kuwa
kunahitajika usawa katika nafasi zinazotolewa na serikali kwa sasa.
Mbele ya wanahabari leo
Jijini Dar es salaam mashirika takribani Kumi yakiongozwa na mtandao wa jinsia
nchini TGNP yanajitokeza mbele ya wanahabari kuzungumzia swala hilo huku
wakionyesha wasi wasi wao juu ya nafasi ya wanawake katika kupewa nafasi za
uongozi hasa hizo za kuteuliwa na Mh Rais.
Mratibu wa kituo cha usuluhushi kutoka TAMWA ambaye ni GLADNESS MUNUO akizungumza katika mkutano huo leo |
Liliani Liundi ni
Mkurugenzi wa Mtandao wa jinsia nchini TGNP akizungumnza na wanahabari amesema
kuwa ukiangalia nafasi za makatibu wakuu utagundua kuwa kati ya 29 walioteuliwa wanaume ni 26 ambao ni sawa na asilimia 89.7
huku wanawake wakipungua kutoka 5(asilimia 21.7) mwaka 2014 hadi 3(aslimia
10.3) kwa sasa hivyo wanawake wamepungua kwa aslimia 10,ambapo kwa upande wa
manaibu makatibu wakuu idadi ya wanawake imepungua kwa kiasi kikubwa pia.
Wawakilishi wa mashirika mbalimbali watetezi wa haki za wanawake wakiwa katika mkutano huo |
Aidha amesema kuwa
katika nafasi za wakuu wa mikoa kwa Tanzania bara kati ya nafasi 26 nafasi 21
wamepewa wanaume ambao ni sawa na asilia 80,na wanawake 5 sawa na asilima 20 ya
mikoa yote Tanzania bara ambapo kwa wakuu wa wilaya bado hali ni hiyo hiyo
ambapo kwa mwaka huu wanawake ni asilima 28.89% ukilinganisha na aslimia 71.1
ya wanaume ambapo inaonyesha kuporomoka ukilinganisha na mwaka jana ambapo
wanawake walikuwa 35.07%.
Amesema kuwa sasa wao
kama wanaharakati wameona kama
wataendelea kuiacha hali hiyo kuendelea
itarudhisha nyuma juhudi ambazo ziloifanywa na serikali za awamu iliyopita ya
kuleta usawa wa kijinsia ambapo ameiomba serikali ya awamu ya tano kuanza
kuwapa kipaumbele wanawake katika nafasi hizo za uongozi.
Mratibu wa kituo cha
usuluhushi kutoka TAMWA ambaye ni GLADNESS MUNUO akizungumza katika mkutano huo
amesema kuwa hakuna serikali duniani ambayo inaweza kufikia malengo yake hasa
ya kimaendeleo bila kuwapa kipaumbele wanawake kwani wao ndio wazalishaji
wakubwa katika taifa lolote duniani.
Ameongeza kuwa katika
uteuzi huo uliofanyika imewasikitisha sana kuona hata katika majina ambayo
yametoka serikali imeshindwa hata kuwagawa na kuonyesha majina na jinsia za
watu jambo ambalo linaonyesha wazi kipaumbele kwa jinsia ya wanawake sio
kipaumbele kikubwa cha serikalio hii.
Mashirika hayo ambayo
ni TAMWA,ULINGO,TAWLA,WAJIKI,WOFATA,TAWIA,WFT,WLAC,LISA,BINTI LEO kwa pamoja wamemtaka
Rais wa Tanzania pamoja na serikalio yake kusimamia kwa vitendo mikataba ambayo
imeseiniwa nan chi hususani inayohusu usawa wa kijinsia ili kupunguza pengo
lililopo kuelekea usawa wa 50 kwa 50 katika nafasi za uongozi.
No comments:
Post a Comment