Baada ya headlines za muda mrefu kuhusu wazo la mfanyabiashara na mwenyekiti wa klabu ya Dar es Salaam Young Africans Yusuph Manji kuomba ridhaa ya kuikodi klabu hiyo kwa kipindi cha miaka 10 kupingwa na baadhi ya watu.
Habari zilizoenea katika mitandao ya kijamii na baadhi ya watu wa ndani ya Yanga leo August 15 2016 ni kuwa mwenyekiti wao Yusuph Manji anajiondoa rasmi na kuachia nafasi ya uenyekiti wa Yanga kwa sababu ya maneno kuwa mengi na kudai kusemwa na wanasiasa kuhusu wazo lake.
Sababu mbili zinazodaiwa kumfanya Yusuph Manji amejiondoe ndani ya Yanga ni kusemwa na baadhi ya viongozi wa serikali na baadhi ya viongozi wa Yanga ambao wanatajwa kutumiwa na baadhi ya wafanyabiashara kwa maslahi yao binafsi, badoManji hajatangaza rasmi kupitia vyombo vya habari.
AIDHA
Baada ya taarifa kwamba Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amejiuzulu uenyekiti kuzagaa, SALEHJEMBE ilifanya kila juhudi kumpata na mwenye akazungumza kwa ufupi.
Alipoulizwa kuhusiana na suala la kujiuzulu na pia kusitiza uamuzi wake wa kutaka kuwekeza au kuikodisha Yanga kwa miaka kumi, alisema basi imetosha.
“Kwa kweli imetosha, imetosha sasa,” alisema.
Alipoulizwa afafanue kuhusiana na kauli hiyo, Manji aliongeza.
“Nimesema hivi, imetosha. Naomba uniache, nisingependa kujibu lolote kwa sasa, niache tafadhari."
Kumekuwa na taarifa kwamba Manji ameamua kuachana na wazo lake la kuwekeza Yanga kwa miaka 10 baada ya kuona hata baadhi ya viongozi wa serikali wakimuandama kwa madai wanatumiwa na baadhi ya mamilionea.
Taarifa nyingine zimeelezwa kwamba, wako wanachama wa Yanga ambao wanaona hawatafaidika na maslahi yao binafsi kama Manji atawekeza, hivyo wamekuwa wakipambana kuhakikisha haingii mkataba na kupewa nafasi hiyo kwa kuwa inaweza kuwavuruga.
Awali, kumekuwa na taarifa Manji ameamua kujitoa kwa kuwa kuna juhudi za chini pia zinazohusisha hadi watu wengine wenye mamlaka katika soka ambao wana hofu na uwekezaji wake.
Source---millad ayyo.com NA sallehe jembe blog
No comments:
Post a Comment