Friday, August 26, 2016

KAMATI YA BUNGE YA TAMISEMI YATEMBELEA MRADI WA MABASI YAENDAYO HARAKA (DART) JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (katikati), akizungumza na wajumbe wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) wakati wa ziara yao ya kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Max Malipo, ambayo imeingia ubia wa utendaji na Udart,  Mhandisi Juma Rajab, akizungumza na wajumbe hao katika ziara hiyo.
  Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (kulia), akiwapatia kadi za kupandia mabasi hayo wajumbe hao.
 Wajumbe wa kamati hiyo wakipita katika eneo la kukatia tiketi kwa kutumia gadi maalumu badala ya tiketi za kawaida.
 Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Anjelina Malembeka (kulia), akiteta jambo na  Esther Mahawe ndani ya basi la mwendo wa haraka Dar es Salaam leo, walipokuwa katika ziara ya kutembelea mradi wa Udart. Wengine nyumba kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza na Mariam Ditopile.
 Wajumbe hao wakiwa ndani ya basi hilo la kampuni ya Udart katika ziara hiyo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Udart, Lonadi Lwakatare akitoa ufafanuzi kwa wajumbe hao.
  Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa (mwenye suti nyeusi mbele), akiwaongoza wajumbe hao katika ziara ya kutembelea makao makuu ya udart.
Mkuu wa Oparesheni wa Chumba cha kuangalia mienendo ya mabasi ya udart yakiwa barabarani, Mhandisi Mohamed Kuganda (kushoto), akitoa maelekezo mbele ya wajumbe wa kamati hiyo jinsi mfumo huo wa kuonesha mabasi hayo unavyofanyakazi.


Na Dotto Mwaibale

Kamati ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa leo asubuhi imefanya ziara ya siku moja ya kutembelea mradi wa Udart yenye lengo la kujua jinsi mradi huo unavyoendeshwa pamoja na kujua changamoto zake ambapo wajumbe hao waliongozwa na Mwenyekiti wao Jasson Rweikiza ambaye ni Mbunge wa Bukoba vijijini.

Katika hatua nyingine ya ziara hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhakikisha anawaondoa wafanyabiashara katika Miundombinu ya Kampuni ya Mabasi ya mwendo wa haraka (Udart)

Simbachawene alitoa agizo hilo wakati akizungumza na uongozi wa Udart baada ya kufanyika majuisho ya ziara ya kamati ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa kutembelea mradi wa Udart Dar es Salaam leo.

"Namuagiza mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuwaondoa mara moja wafanyabiashara katika miundombinu ya udart" alisema Simbachawene.

Mkurugenzi Mkuu wa Udart, David Mgwassa alisema changamoto kubwa iliyopo ni elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya miundombinu ya udart.

Alisema changamoto waliyonayo ni wananchi kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu matumizi ya miundombinu ya udart ambapo wamejipanga kuhahikisha kila mwananchi anaipata jambo litakalosaidia kuitunza na kuendelea kupata huduma bora.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza aliutaka uongozi wa udart kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora za usafiri jijini Dar es Salaam ili kuwapunguzia adha ya usafiri wananchi.

Kamati hiyo ilitembea mradi wa udart katika vituo vikuu vya Kimara mwisho, Moroco makao makuu ya Udart Jangwani, Gerezani na Kivukoni.

No comments: