Wednesday, August 3, 2016

KITUO CHA TELEVISHENI CHA TV 1 KURUSHA MATANGAZO YA LIGI KUU SOKA YA UINGEREZA EPL

 Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi (katikati),akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ,Kituo cha  Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti  13 mwaka huu. Kulia ni Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu na Meneja Masoko Startimes, kushoto ni Felix Awino 
 Meneja Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu ,Kituo cha  Televisheni cha TV1 Tanzania kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti  13 mwaka huu. Kushoto ni Mkuu wa TV 1, Joseph Sayi na kulia ni Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah.  
 Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey Abdallah (katikati), akizungumzia masuala ya mpira katika mkutano huo.
 Production Meneja wa TV 1, Mukhsin Khalfan Mambo akizungumza katika mkutano huo.
 Mkutano ukiendelea.
 Wanahabari wakiwa kazini.
 Taswira ya meza kuu katika mkutano huo.
 Mchambuzi wa michezo, Ally Kashushu (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Mmiliki wa Blog ya Kajuna Son, Cathibert Kajuna (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
 Wapiga picha za habari wakiwa kazini.
 Baadhi ya wafanyakazi wa TV 1 wakiwa wakifuatilia matukio mbalimbali ya mkutano.
Mkutano ukiendelea.



Na Dotto Mwaibale

KITUO cha  Televisheni cha TV1 Tanzania kinatarajia kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mpira wa miguu ya ligi kuu soka ya Uingereza EPL matangazo ambayo yanatarajia kurushwa kuanzia Agosti  13 mwaka huu.

Ligi kuu soka nchini Uingereza ndio ligi maarufu zaidi duniani na hii ni kutokana na kushirikisha timu kongwe zenye ubora na mashabiki dunia nzima ikiundwa na timu maarufu duniani kama vile Manchester United,Liverpool, Arsenal pamoja na Chelsea.

TV1 Tanzania ndio kitakuwa kituo pekee cha runinga hapa nchini kupewa haki za kurusha matangazo haya yatakayokujia moja kwa moja yaani Live yakihusisha pia uchambuzi wa ligi hiyo ambapo kutakuwa na vipindi vya kabla ya mechi na baada ya mechi husika.

Kwa upande Mkuu wa Kituo cha TV 1 Tanzania  Joseph Sayi alisema  hii ni fursa kubwa kwa wadau wa soka hapa nchini kuishuhudia ligi hiyo moja kwa moja, Mkuu wa kitengo cha masoko wa TV1 Gillian Rugumamu alisema lengo ni kuwapelekea watazamaji wao wa Tanzania ligi kuu England ambayo ni ligi inayopendwa na kufuatiliwa na Watanzania.

Baadhi ya watangazaji na wachambuzi watakaokuwa wakishiriki katika urushaji wa matangazo  hayo na uchambuzi ni Ally Kashushu na Dkt. Leakey Abdallah ambaye ni mchambuzi mwenye uzoefu wa miaka 20 kwenye tasnia ya michezo husasani uchambuzi.

Mchambuzi wa Michezo Dk. Leakey alisema watanzania wategemee uhondo wa ligi hiyo kutokana na uwepo wa wachezaji nyota na makocha mahiri kama Antonio Conte,Arsene Wenger,Jurgen Klopp na makocha hasimu Jose Mourinho wa Manchester United na Pep Guardiola wa Manchester City.

Tv1 Tanzania ni kituo cha runinga kilianza mwaka 2013 ambapo  kilianza kurusha matangazo yake rasmi  Januari 2014 ambapo kimekuwa kikiandaa na kurushwa vipindi vyenye ubora wa hali ya juu ambapo TV 1 inapatikana kupitia ving’amuzi vya Startimes namba 103,Azam 119 na Ting 36.

No comments: