Kikao cha pamoja cha Kamati Kuu na wabunge wa CHADEMA kilichokuwa kikifanyika Giraffe Hotel Mbezi Beach, Dar es Salaam kimevamiwa na kuvunjwa na Jeshi la Polisi.
Viongozi wote, akiwemo Edward Lowassa na Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Vicent Mashinji, wabunge na wajumbe wa Kamati Kuu wamepelekwa Kituo cha Polisi cha Kati.
Akizungumzia kukamatwa kwa viongozi hao Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema waliokamatwa na polisi kwa ajili ya mahojiano ni Edward Lowassa, Freeman Mbowe, John Mnyika, Dk Vincent Mashinji na Said Issah.
No comments:
Post a Comment