Kiongozi wa Kataa Unene Family Bi Angela Msangi (katikati) akiwakaribisha wanachama wenzake wa Kataa Unene Family wakati wa maadhimisho ya miaka mitatu ya KUF yaliyofanyika Jumapili Agosti 7, 2016 jijini Dar es Salaam. Pembeni kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Nidhani ya KUF, Bi. Etty Kusiluka na Bi. Mariam Sagini (kushoto) Mshindi wa shindano la kupunguza kilo 10 kwa muda wa miezi mitatu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akizungumza na wanachama wa Kataa Unene Family (KUF) jumapili Agosti 7, 2016 wakati wa maadhimisho ya miaka 3 tokea umoja huo kuanzishwa. Pembeni kulia ni Kiongozi wa Kataa Unene Family Bi. Angela Msangi na Bi. Mariam Sagini Bi. Mariam Sagini (kushoto) Mshindi wa shindano la kupunguza kilo 10 kwa muda wa miezi mitatu.
---
Kundi la Kataa unene (KUF) linalojihusisha na kupunguza unene kwa mazoezi na kula vyakula bora limeadhimisha miaka 3 kwa na kuweka mikakati mipya ya kuwasaidia wengine.
Akizungumza katika sherehe hiyo iliyofanyika Epidor Masaki, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda ambaye alipita kuwasalimia alilipongeza kundi hilo huku akisema kuwa afya ni msingi wa maendeleo yoyote duniani, hivyo hatua ya kutambua kujiweka imara mapema ni njema.
"Nawapongeza sana kwa moyo mlionao wa kufanya mazoezi si jambo dogo maana linahitaji nidhamu ya hali ya juu ... kujisimamia mwenyewe bila kushinikizwa na mtu,' alisema Mhe. Makonda.
Aidha, alieleza kuwa viwanja vya michezo jijini Dar es Salaam vipo vingi, maeneo ya wazi pia hivyo kuwasihi wananchi kujihusisha katika mazoezi, huo wao kama viongozi wakiwaunganisha na makundi mengine ya michezo kwa mashindano kama Toto cup, Ndondo cup na mengineyo, hasa wanafunzi wa vyuoni na shule za msingi.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Kataa Unene Family Bi Angela Msangi alisema katika miaka mitatu, tayari watu zaidi ya 40 wamepunguza kuanzia kilo 15 hadi 25, ambapo tayari watu 10 wamefikia malengo ya kilo zinazohitajika kutokana na urefu wao na wanaendelea kujidhibiti.
Angela alisisitiza kuwa, kupungua kwa kufanya mazoezi na kula vyakula vinavyofaa na kushauriwa kunawezekana endapo tu mtu ataamua kujikana na kudhamiria,akiwaondoa watu fikra potofu kuwa wanaopungua wanatumia dawa.
Shughuli hiyo ya Kataa Unene ilienda sambamba na kutoa zawadi kwa waliofanya vizuri katika shindano la kupungua la miezi mitatu iliyopita, lililopewa jina la Sagini challange,ambapo aliyeibuka kinara wa shindano hilo ni muasisi wa shindano Mariam Sagini, aliyepunguza kilo 10 tangu mwezi Mei mwaka huu.
Bi. Mariam akiwaonyesha wenzake jinsi gauni lake lilivyomkaa vyema baada ya kupungua kilo 10 kwa muda wa miezi mitatu.
"Yani mwenzako nimejaribu mara tatu"
Wanachama wa KUF wakibadilisha mawazo.
Wanachama wa KUF wakipongezana.
Wajumbe wa Kamati ya Nidhamu ya KUF, Bi. Etty Kusiluka (kushoto na Bi. Ester Ulaya Cathbert (kulia) wakibadilishana mawazo wakati wa sherehe ya maadhimisho ya miaka mitatu.
Kila mwanachama aliweza kupata nafasi ya kuelezea changamoto na mafanikio yake.
Mjumbe wa Kamati ya Nidhamu Bi. Eter Ulaya Cathbert akitoa machache.
Wanachama wa KUF wakipeana zawadi.
Kiongozi wa Kataa Unene Family Bi Angela Msangi akitoa shukrani kwa wanachama wote walioweza kufika katika maadhimisho hayo.
.
Wanachama wa KUF wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda.
No comments:
Post a Comment