Mkuu wa wilaya ya ILALA,SOPHIA MJEMA,amewataka
wafanyabiashara katika soko la kariakoo kutoandamana siku ya tarehe moja mwenzi
wa tisa.
Akizungumza na wafanyabiasha hao hii leo jijini Dar-es-salaam
katika zoezi la usafishaji mazingira linalofanyika kila jumamosi ya mwisho wa
mwenzi,amemewataka wafanyabiashara hao kutojihusisha katika maandamano ya
tarehe moja mwenzi wa tisa yajulikanayo
kama UKUTA,
“nawaomba wafanyabiashara msiandamana siku hiyo kwani
maandamano hayo hayana matiki wala na hayafuati sheria na katiba ya nchi
iliyopo nawaomba siku hiyo mfanye bishara zenu kwa utulive na amani" Kiongozi
huyo amesema .
Pia MJEMA ametembelea hospital ya Amana akiwa na wakuu wa
idara mbalimbali katika manispaa hiyo na kushiriki zoezi la usafishaji wa
mazingira katika hospitali hiyo amewataka wauguzi na madaktali kuwa na
utamaduni wakufanya usafi wa mara kwa mara
“ili wagonjwa
wapate matibabu bora na afya njema awanabudi kukaa kwenye mazingira
yaliyo safi hivyo natoa wito kwenu zoezi hili la usafi lisiishie hapa bali lifanyeni
kila wakati ilikupunguza magonjwa mbalimbali ya mlipuko nchin"amesema.
Aidha diwani wa kariakoo,MASAMAKI,amewataka wananchi
kujijengea utamaduni wakufanya usafi wenyewe bila kushurutishwa,kwan wakifanya
ivyo watasidia kuondoa magonjwa mbalimbali ya mlipuko,pia amewaasa kufuata
sheria na taratibu za nchi zilizopo
No comments:
Post a Comment