Mfanyakazi wa Kituo cha
Sheria na Haki za Binadamu Nchini Lhrc GELINE FUKO ambaye alipata Bahati ya
kuwakilisha watanzania katika warsha maalum iliyoandaliwa na Rais wa marekani
Barack Obama iliyokuwa na lengo la kuwakutanisha watu mbalimbali wakiwemo wanaharakati
duniani wenye mawazo makubwa na mazuri ambapo kwa Tanzania GELINE FUKO ndiye
aliyewakilisha amerejea nchini usiku wa kuamkia leo na kupata mapokezi makubwa
kutoka kwa wafanyakazi wenzake wa kutio hicho na watanzania wengine.
Geline Fuko ndiye
aliyewasilisha wazo la kuanzishwa kwa Kanzi Data Maalum ndani ya Kituo cha LHRC
ambayo ni maalum kwa ajili ya katiba ya Tanzania ambayo inawapa nafasi
watanzania wote kupitia na kusoma katiba yao kupitia Data Base hiyo maalum na
pia habari mbalimbali kuhusu mchakato wa katiba nchini wazo ambalo limempa nafasi ya kushiriki katika
warsha hiyo nchini marekani na kumfanya kujiletea sifa lukuki kwake na kwa
Taifa kwa ujumla.
Katika shughuli hiyo
moja kati ya mambo ambayo yaliwawavutia watu wengi ni pamoja na Rais Obama
kumtaja Mtanzania huyo kama moja ya wanaharakati ambao amevutiwa na wazo lake
la kuanzisha Kanzi Data ya katiba na
kumpa nafasi ya kutembelea maeneo mbalimbali na kujifunza Zaidi nchini Humo.
Akizungumza na
wanahabari mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa Mwalimu
Nyerere Dar es salaam GELINE amesema kuwa Wazo lake la kunzishwa kwa kanzi data
ambayo imekuwa ina maswala yote kuhusu katiba na kuwapa watanzania wanafasi ya
kusoma katiba yao kwa njia rahisi Zaidi wazo ilo lilitajwa na Rais Obama kuwa
ni wazo bora na kuwazidi wengine waliokuwa wanatoka nchin mbalimbali.
Amesema kuwa Baada ya
Obama kumtaja alipewa nafasi mbalimbali za kipekee ikiwemo yafasi ya kusoma
katika vyuo vikuu viwili nchini marekani na kufundishwa na Maprofesa wakubwa
nchini Marekani,nafasi ya kukuaa na Marais kadhaa wastaafu wa nchini Marekani
na kujifunza maswala mbalimbali kutoka kwao ambapo amesema ni bahati kubwa sana
kwa mwanamke wa kitanzania kama huyo kuipata.
Naemi Silayo ambaye ni
Mfanyakazi wa LHRC akizngunza katika mapokezi hayo amesema kuwa nafasi ya
kwenda kushiriki katika warsha hiyo ilikuwa ni ngumu kupatikana kutokana na
wingi wa watu waliokuwa wanaomba Africa na duniani kote lakini kutokana na
ubora wa Wazo la GELINE alipata nafasi hiyo Adimu ya kuwakilisha watanzania
wengine wote.
Wakizungumza katika mapokezi
hayo baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa kituo hicho cha LHRC akiwemo
mwanasheria PATIANCE MLOWE na Mkurugenzi wa fesha na utawala EZEKIEL MASANJA pamoja
na kumpongeza kwa wingi sana Mfanyakazi mwenzao pia wamesema kuwa jambo hilo ni
ishara ya kuwarudisha watanzania katika mjadala wa katiba mpya ambao
umesahaulika kwa kipindi kirefu sasa na kuanza upya upatikanaji wa katiba kwa
nchi ya Tanzania
No comments:
Post a Comment