Wednesday, August 10, 2016

Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla apongeza utafiti wa Twaweza katika masuala ya Afya nchini

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla amepongeza utafiti wa wadau juu ya Sekta ya Afya hapa nchini ambapo amesema tafiti hizo zinasaidia Serikali katika kupanga mipango yake thabiti na kufahamu wapi panamapungufu ilikuchukua hatua zaidi.

Akiuzungumza wakati wa uzinduzi wa Utafiti wa Twaweza ‘ Sauti za Wananchi, Dk. Kigwagalla amesema kuwa, Serikali ya awamu ya tano, imejipanga kusaidia wananchi kupitia sera za Afya hivyo kila mwananchi atapata huduma bora za Afya hapa nchini licha ya changamoto zilizopo Wizara ya Afya ipo katika kuboresha mifumo yake mbalimbali ikiwemo suala la bima ya Afya kwa kila mtanzania na huduma bora za Afya kuanzia ngazi ya chini.
Miongoni mwa mambo yaliyobainika katika tafiti hiyo ya Twaweza ni pamoja na muitikio mkubwa wa watoa huduma wakiwemo Madaktari na Manesi kutoa huduma bora bila vikwazo kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

“Matokeo haya ya Twaweza yameonyesha matokeo mazuri hii ni pamoja na huduma nzuri ikiwemo lugha ya kiutendaji kwa sasa imekua ni ya kiungwana zaidi tofauti na kipindi cha nyuma. Serikali ya awamu hii ya tano imekuwa ikifanya kazi kwa kasi sana kwa sasa hatukai maofisini zaidi muda wote ni kazi tu” alieleza Dk. Kigwangalla.

Kwa upande wake Afisa mipango wa Twaweza, Bi. Nelline Njovu amesema kuwa Twaweza wamezindua matokeo ya utafiti huo ambao uliendeshwa kwa njia ya simu katika mfumo wa Afya ambapo waliangalia mambo mbalimbali ikiwemo juu ya Maboresho ya Huduma za Afya kwa mwaka 2015-16 ambayo yanajumuisha Serikali ya awamu ya tano tokea kuingia madarakani.

Utafiti wa Sauti za Wananchi wa Twaweza unaonyesha maoni chanya kutoka kwa wananchi juu ya sekta ya afya nchini Tanzania. Kwa mfano, ni asilimia 18 wananchi wanaoripoti kuona upungufu wa madaktari katika vituo vya afya miezi mitatu iliyopita, ukilinganisha na asilimia 43 walioliona tatizo hili mwaka 2015.
DSC_4896Baadhi ya wadau wakifuatilia mkutano huo wa Twaweza mapema leo Agosti 10.2016, Jijini Dar es Salaam wakati wa utoaji wa taarifa za tafiti upande wa Afya.
DSC_4891 DSC_4899
Profesa Kitila Mkumbo akitafakari jambo wakati wa tukio hilo.
DSC_4901
Wadau wa Twaweza wakitoa maoni yao
DSC_4910
Wadau wa Twaweza wakitoa maoni yao
DSC_4926 DSC_4932
Afisa mipango wa Twaweza, Bi. Nelline Njovu akifafanua jambo katika tikio hilo
DSC_4904
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akinukuu baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa kwake juu ya masuala ya Afya katika tukio hilo..
DSCS_4874
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akifafanua jambo juu ya Wizara yake ya Afya ilivyojipanga kutatua kero za wananchi kupitia huduma za Afya bora.

No comments: