Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla mapema siku ya Agosti 11.2016 amekutana na wadau wa Sekta ya Afya kutoka taasisi Touch Foundation kuangalia namna ya kusaidia sekta ya Afya hasa kwa maeneo ya pembezoni mwa Nchi ili kuimalisha hudumm hizo.
Ugeni huo kutoka katika Taasisi ya Touch Foundation ya nchini Marekani umeonyesha nia yake ya dhati ya kuendelea kusaidiana na Wizara ya Afya ya Tanzania ikiwemo huduma za akina mama Vijijini.
Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla amekutana na ugeni huo ofisini kwake ukiongozwa na Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya Touch Foundation ambae pia ni mstaafu kutoka katika kampuni ya McKinsey, Bwana. Lowell Bryan ambaye pia alishawai kuwa mshahuri kwa miaka mingi huko kipindi cha nyuma katika masuala ya Afya ya Tanzania.
Ujumbe wa ugeni huo una miradi mbalimbali kama kuzalisha wataalam wa afya, kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto kwa kuboresha mfumo wa rufaa kutoka kijijini kuja mpaka mahala watakapopata huduma na kwa sasa wameanza na wilaya mbili za Sengerema na Shinyanga Mkoani Shinyanga.
Akielezea muda mfupi baada ya majadiliano na ujumbe huo Dk. Kigwangalla alibainisha kuwa Wameonyesha nia ya kuendelea kuisaidiana na Tanzania katika masuala ya Afya hivyo mikakati ya itaendelea kuwa endelevu hasa katika miradi ya kusaidia kupunguza vifo kwa akina Mama Wajawazito.
“Mradi wao wa kupunguza vifo vya wakinamama wajawazito pamoja na watoto, unatekelezwa kwa kuboresha mfumo wa rufaa kutoka kijijini kwa wakinamama wajawazito kuja mpaka wanapoweza kupata huduma za kiafya hii ni pamoja na Kituo cha Afya ama Hospitali kubwa.
Wametengeneza utaratibu wa usafiri, mawasiliano ya simu na kuwapatia wahudumu posho katika Wilaya ya Sengerema na shinyanga wakishirikiana na Vodafone Foundation.
Watatusaidia kutengeneza mikakati ya kiufundi ya namna ya kuboresha huduma za afya ya msingi, huduma hizi za msingi ni kama vituo vya afya na zahanati ikiwa ni pamoja na kutupa utaalam katika eneo la kufanya tathmini ya rasilimali watu katika sekta ya afya, kuanzia gharama za kuajiri madaktari ama kada za chini” aliongeza Naibu Waziri Dk. Kigwangalla.
Na Hashim Ibrahim (UDSM-SJMC).
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla akisikiliza jambo kutoka kwa wageni (Hawapo pichani) wakati wa mazungumzo juu ya uwekezaji wa katika sekta ya Afya.
Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya Touch Foundation ambae pia ni mstaafu kutoka katika kampuni ya McKinsey, Bwana. Lowell Bryan akimsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla (Hayupo pichani).
Ugeni katika mkutano huo
Majadiliano yakiendelea
Bwana. Lowell Bryan akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla wakati wa mkutano huo uliofanyika ofisini kwa Naibu Waziri, Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment