Monday, August 22, 2016

RITA SASA KUZIFUTA BODI ZA UDHAMINI ZENYE MAKOSA,WAZIRI MWAKYEMBE ATOA NENO,SOMA HAPO KUJUA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhpt83o7KuuYs3GwLbSY1tS_Mfa49_t77zkkLPxns6s0J-43ADukLVcukPFVd2kNWOM44fZUkswG3JT4JBtm-qfHC0z5PT7p8jo6tJ3i6EElWMv75o-6ETg9rdCWBLr7V8hpesCOxMLz4U/s640/4.JPG

Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam
 
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgOjW3l6hGHYF494gRqcIdiei1OZ33WUFi7UJX2H5Z5CdSQPRuQEDDQxJOzlboDuK4fIh3peIzvL6qBAGNouGe-ZKfwNuYwMcJr4jWtkhsARchRMHb6Kz2XToqAbmfUJ9WTe2D04owiRH0/s640/1.JPG
Waziri wa Katiba na sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na  waandishi wa habari hawapo pichani katika mkutano wa kupokea ripoti ya  ukaguzi kutoka kwa Taasisi zote zinazofanya usajili wa asasi za kiraia leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Katiba na Sheria Amon Mpanju.


SERIKALI imesema itaendelea kuzikagua  bodi za udhamini zilizochini ya taasisi ya wakala wa ufilisi na  udhamini (RITA)ilikuzibaini taasisi hewa na zile zilizosajiliwa Kisheria na bodi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es salaam Waziri wa katiba na Sheria nchini Dk.Harrison Mwakyembe amesema kuwa ukaguzi huo wa bodi yaudhamini unalenga kuzitambua taasisi zinazotambulika na Rita .

''Tunataka tubakie na asasi za kiraia zilizo sajiliwa ambazo zinatambulika kisheria ambapo nimelezwa kuwa kuna taasisi ambazo hazikufuata utaratibu wa usajili hivyo basi ninazitaka asasisi za kiraia zilizosajiliwa na zinazo tambulika tu ''Amesema  Waziri wa Katiba na sheria Dk.Harrison Mwakyembe .


KATIKA hatua nyingine Msajili wa asasi za kiraia nakidini katika wakala wa ufilisi na udhamini (RITA) Mery Komba amesema kuwa katika taarifa bodi ya wadhamini  takribani bodi za wadhamini 1944 kati ya 5262 zilizowasilisha tarifa zao kwa njia ya barua pepe na zingine kwakuwasili ofisini .

Alisema kuwa katika majalada yaliyo chambuliwa 5262 kati ya majalada 4287 yalichambuliwa na kuwekwa kwenye kanzi data ambapo bodi za wadhamini mini 500 zilikuwa mfu .

''KATIKA tangazo liliotolewa mei 17 mwaka huu kwenye gazeti la serikali la daily NEWS na mwananchi kwa muda wasiku 30 jumla 200 kati taasisihizo ni20 tu ndizo ziliweza kutekeleza agizo huku taasisi 180 zilibainika kutekeleza wajibu wake ''Alisema  Mery Komba .
 
Gega Nancy
Alisema pamoja nahatua hiyo pia taasisi hiyo imeandaa mpango mkakati wakuzifutia taasisi 320 agizo hilo linatarajiwa kutekelezwa mwishoni mwamwezi agost mwaka huu.
 
Chanzo FULLHABARI BLOG

No comments: