Katikati ni Mratibu wa mashindano hayo Masudi Kandoro kutoka kampuni ya High Time Marketing and Promotion ambao ndio waandaaji wakuu wa shindano hayo amkzumgumza na wanahabari mapema leo wakati wa kutangaza Shindano hilo(PICHA NA EXAUD MTEI) |
Kwa mara ya kwanza
nchini Tanzania na katika Historia ya music hatimaye mashiundano ya kwanza ya
kumtafuta mwanamuziki na mwimbaji wa music wa singeli yamezinduliwa nchini
mashindano hayo yakilenga kumpata msanii mwenye uwezo wa kuimba music wa
kisingeli mashindano ambayo yamepewa jina la STAR WA SINGELI.
Mashindano hayo ya
kuimba singeli nchini Tanzania yanalenga kuibua vijana wenye vipaji vya hali ya
juu ambao wako mitaani nia ikiwa ni kuwainua na kuwafanya kuwa wanamusic
watakaotambulika ndani na nje ya Tanzania huku pia ikiwa ni njia moja wapo ya
kutengeneza ajira zenye staha kwa vijana wa Dar es salaam.
Akizungumza na
wanahabari wakati akitangaza kuanza kwa mashindano hayo mbele ya wanahabari Masudi
Kandoro kutoka kampuni ya High Time Marketing and Promotion ambao ndio
waandaaji wakuu wa shindano hilo amesema kuwa mashindano hayo yatafanyika
katika Jiji la Dar es salaam tu na
mashindano hayo yamegawanywa katika sehemu nne ambazo ni Kinondoni,Ilala,Temeke,na
Kingamboni ambapo kila sehemu kutafanyika mchujo kwa awamu mbili.
Ameongeza kuwa awamu ya
kwanza itakuwa katika viwanja vya wazi kila sehemu itatoa washindani 12 kisha
awamu ya pili sehemu mbili zitaungana katika mashindano ya ndani nya ukumbi
ambapo kinondoni itaungana na ilala wakati temeke ikiungana na kigamboni.
Akizungumza kuhusu
fainali na washindi wa shindano ilo la STAR WA SINGELI amesema kuwa fainali za
mashindano hayo zitafanyika siku ya jumamosi ya tarehe 10/09/2016 katika
viwanja vya Dar Live Dar es salaam kuanzia saa moja usiku ambapo siku ya
fainali atapatikana mshindi mmoja kwenye washindi 12 watakaokuwa wanawania
nafasi hiyo ambapo mshindi atajinyakulia zawadi ya million kumi.
Wanahabari wakichulkua Taarifa Hiyo |
Akizungumzia mgawanyo
wa Million Kumi hizo za mshindi wa kwanza amesema kuwa mshindi hatapewa Kiasi
icho chote bali kitagawanywa katika maeneo kadhaa ikiwemo kupata usimamizi wa
misic chini ya HIGH TIME,Kurekodi album ya music Audio,Kufanyiwa Video tatu
zenye viwango vya kimataifa,Kutangaza Music wa mshindi ndani na nje ya mipakaya nchi pamoja na kupewa kiasi
cha Pesa Taslim.
Katika fainali hizo
zitakazofanyika Dar Live zinatarajiwa kupambwa na star wa music huo mzee wa
Hainaga Ushemeji Man Fongo na wasanii wengine wakali ambao wanaendelea na
mazunguzo kushiriki.
No comments:
Post a Comment