Katika kuadhimisha
miaka 40 Tangu kuanza kutoa Huduma kwa mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia
TAZARA,wameandaaa maonyesho maalum yatakayofanyika katika makao makuu ya
mamlaka Hiyo Jijini Dar es salaam kuanzia Tarehe 24-26 ya mwezi huu yakiwa na
lengo la kuonyesha huduma na utendaji kazi wake kwa kipindi chote cha utoaji wa
huduma yao.
Katika Taarifa
iliyotolewa kwa wanahabari kutoka kwa Mkurugenzi mtendaji wa TAZARA Bwana Bruno
Tandeo Chin’gandu imeeleza kuwa katika
maonyesho hayo watanzania watakaotemebea hapo watapata nafasi ya kujadili
mijadala mbalimbali ikiwemo changamoto zinazokumba Sekta hiyo ya usafiri wa Reli
nchini Tanzania ambapo wadau mbalimbali kutoka kila kona ya sekta hiyo
watakuwepo kutoa Uzoefu wao juu ya maswala mbalimbali yakiwemo ya kisera,ya
usafiri wa reli nchini.
Taarifa hiyo pia
imeeleza kuwa maadhimisho hayo ya miaka 40 yamekuja ikiwa si tu Tazara kueleza
changamoto zake bali yamekuja kipindi ambacho Tazara imekuwa ikipigana
kuhakikisha kuwa inasonga mbele kwa nguvu na kukabiliana na changamoto zote
huku Taarifa hiyo ikiwakaribisha watanzania wote kutembelea maonyesho hayo
yatakayoanza Tarehe 24 kujionea huduma na bidhaa mbalimbali zitolewazo na
mamlaka hiyo.
Maadhimisho ya miaka 40
yameanza takribani miezi miwili iliyopita ambapo wamekuwa wakifanya shughuli mbalimbali
kama Usafi katika maeneo mbalimbali katika Jamii na mahospitalini,kuchangia
Damu kupitia mpango wa damu salama nchini,pamoja na kuwapokea wanafunzi na
kuwaelekeza mambo mbalimabli juu ya Treni yao ya Abiria,
No comments:
Post a Comment