STORY NA VICENT MACHA
Mkurugenzi wa mtandao
wa jinsia nchini Tanzania TGNP Lilian Liundi amesema kuwa mfumo mpya wanaotumia
sasa wa kutoa elimu kwa wananchi jinsi gani wanaweza kushiriki katika harakati
za kujipatia maendeleo ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa kuhoji maswala
mbalimbali kwa viongozi wao (Uraghibishi) umefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika
wilaya saba walizofanya.
Akieleza zaidi juu ya
mfumo huo amesema kuwa uraghbishi
ulianza toka mwaka 2012 na waliweza kuzifikia
wilaya saba ambazo ni Kinondoni, Ilala, Temeke, Kisarawe, Mororgoro vijijini,Mbeya
vijijini na Kishapu huku pia wakiweza
kuvifikia vikundi zaidi ya 220, wakiwemo wanaume zaidi ya 1000 na wanawake
zaidi ya 3000 huku akisema kuwa zoezi hilo linaendelea ili kuwafikia watanzania
wengi zaidi.
Ameeleza kuwa njia hiyo
imefanikiwa kusaidia kwa kiwango kikubwa
kuweza kuleta maendeleo kwa kuwa
wananchi wengi hawakujua nini wanatakiwa kukifanya endapo serikali imekwama
kuwaletea maendeleo.
Akitolea mfano katika
maeneo kadhaa maeneo kadhaa amesema kuwa ilikuwa mama mja mzito akitaka kwenda
kujifungua inabidi aende na ndoo ya maji kwa kuwa zahanati hazina maji huku pia mama mjamzito akitakiwa aende na mafuta
ya taa au tochi la sivyo atajifungulia gizani. Lakini baada ya kufanya uraghbishi wananchi wengi walijitoa na kuweza
kujichagisha hatimaye kuweza kusogeza huduma karibu kama maji na kupunguza adha
ya kwenda na vitu kama mafuta ya taa au ndoo wakati wa kujifungua.
Aidha katika mafanikio
mengine ambayo ameyataja yaliyoletwa na njia hiyo iliweza kufanya kazi kwa baadhi ya maeneo kama
shinyanga ambapo palikuwa na shule lakini hakuna vyoo ikasababisha wanafunzi na
walimu kuweza kujisaidia vichakani hali ambayo si nzuri kwa afya zao kwani
walikuwa wakizalisha magonjwa ya milipuko. Lakini waliweza kuchangishana fedha
na kati yao walikuwepo mafundi na wakaweza kupata huduma ya vyoo japo kuwa
havikuwa vinatosha lakini viliweza kusaidia ikiwa ni pamoja na mradi wa maji
uliowekwa na wana nchi wakisaidiwa na wahisani waliokuwa wakiona adha hiyo kwa
wananchi wa maeneo hayo.
Mafanikio hayo
ameyataja ikiwa ni ni siku ya pili na ya mwisho toka warsha maalum ya wanahabari ianze ambayo mtandao
wa jinsia Tanzania TGNP uliwakutanisha wanahabari mbalimbali nchini kwa lengo
la kuwaelimisha na kutanua uelewa wao juu ya bajeti yenye mlengo wa kijinsia na
uraghbishi pamoja na kutilia mkazo au kuhamasisha wananchi kuweza kuhusishwa
kwenye upangaji wa bajeti katika ngazi
ya vijiji au kata na mpaka ngazi ya halmashauri na sio viongozi wachache
kuwasemea ambapo warsha hiyo iliongozwa na wadau mbalimbali wa maswala ya
kijinsia akiwemo mkurugenzi huyo wa TGNP
No comments:
Post a Comment