Wednesday, August 17, 2016

WAZIRI MWIGULU AFANYA MAZUNGUMZO NA WATENDAJI WA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA LA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA NA UHALIFU (UNODC)

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(katikati), akizungumza na watendaji wa  Shirika la Umoja wa  Mataifa la Kupambana na Dawa za  Kulevya na Uhalifu(UNODC),  Bi. Kaitlin Meredi (kulia) na  Johan Kruger(kushoto), walipomtembelea ofisini kwake,jijini Dar es Salaam,leo. Ziara hiyo ikiwa na lengo la kujadili njia muafaka za kukabiliana na biashara, matumizi na athari za dawa za kulevya kwa jamii. 
Mratibu  wa Programu ya  Kupambana na Uhalifu wa Majini kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), Kaitlin Meredith (kulia), akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, masuala yanayohusu  udhibiti wa uhalifu unaofanyika majini walipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam, leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati),akiagana na Mratibu  wa Programu ya  Kupambana na Uhalifu wa Majini, Kaitlin Meredith, mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwa waziri,  jijini Dar es Salaam, leo.Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Biashara Haramu ya Dawa za  Kulevya kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), Johan Kruger (Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

No comments: