Raundi ya tatu ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Septemba 3, 2016 kwa michezo minne wakati kwa Jumapili Septemba 4, mwaka huu kutakuwa na mchezo mmoja tu kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyotolewa na Bodi ya Ligi (TBLB).
Michezo ya kesho ni kati ya Mbao FC na Mbeya City utakaofanyika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati Kagera Sugar itazindua uwanja wa nyumbani kwa kucheza na Mwadui ya Shinyanga.
Majimaji itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Majimaji huko Songea na African Lyon itakuwa mgeni wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Mchezo wa Jumapili utakuwa ni kati ya Stand United na Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.
Ligi hiyo ambayo kwa sasa inaongozwa na Azam FC itaendelea Jumatano kwa michezo mitatu ambako mabingwa watetezi Young Africans watakaribishwa na Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Azam ambayo kwa sasa inangoza ligi hiyo itasafiri hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine ilihali Simba itakipiga na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment